Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Samson R. Wambura ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kisangura ,imefanya Ziara ya Kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi Wa Matundu 28 ya Vyoo vya program ya usafi wa mazingira na usambazaji wa Maji vijijini (SWASH-SRWSSP) Katika shule ya Msingi Park Nyigoti.
Shule ya Msingi park Nyigoti ni shule jumuishi yenye darasa la Awali hadi darasa la saba. Shule ina jumla ya wanafunzi 570.Fedha kwa ajili kutekeleza mradi huu zilipokelewa tarehe 05/07/2021 kiasi cha Tshs.35,301,125.56. Serikali na wananchi walitoa michango kwa ajili ya kutekeleza mradi huu ambao umekamilika na umeanza kutumika.
Kamati imeipongeza Kamati shule na uongozi wa kata na kijiji kwa usimamizi mzuri wa mradi na ushirikishwaji wa wananchi na kuwataka kuutunza mradi huo.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti