Semina ya siku tatu kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata Jimbo la Serengeti imehitimishwa rasmi leo Agosti 6,2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Walimu (TRC) Wilayani Serengeti.
Akihitimisha Semina hiyo Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi katika Jimbo la Serengeti Wakili wa Serikali Veronica Lukanda amewataka washiriki wa semina hiyo ambao ni Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata kuhakikisha wanazingatia mafunzo waliyopata kwa siku hizo tatu na kuwataka kuishi kiapo walichoapa siku ya kwanza ya semina hiyo.
Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Serengeti Ndugu. Nyora Elias Chama amewapongeza washiriki wa Semina hiyo kwa nidhamu waliyoionesha wakati wa mafunzo na kuwasisitiza kutanguliza uadilifu katika kila jambo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Semina kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata iliyodumu kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kituo cha Walimu (TRC) ilianza Agosti 4 Mwaka huu na kutamatika leo Agosti 6.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti