• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Mkataba wa Huduma Kwa Mteja

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI

MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

 

                                                                                                                                                                                                      

KAULI YA MKURUGENZI MTENDAJI WA WILAYA

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ni chombo cha Serikali kilichoundwa chini ya  Serikali za  Mitaa, Sheria Na. 7 ya 1982.

Majukumu makuu ya chombo hiki yameainishwa katika Kifungu Na.III cha Serikali hiyo. Kwa ujumla  wake majukumu ya Taasisi hii  kama ambavyo yameorodheshwa  katika Kifungu  cha III cha Sheria  niliyoitaja yanaweza  kuwekwa  makundi makuu yafuatayo:-

  • Jukumu la kimaendeleo
  • Jukumu la Kiuongozi na Utawala
  • Jukumu la Kiuwakilishi.

Katika kutekeleza Majukumu hayo, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti inao  Mpango Mkakati (Serengeti District Strategic Plan ……………….. ambao Dira yake ni :-

Kushirikisha  Jamii na Wadau wengine kutumia  Rasilimali zilizopo katika  kuboresha Huduma endelevu za  Kiuchumi na Kijamii. Mipango yetu ni  kujiimarisha  kutoa Huduma  endelevu za Kiuchumi na Kijamii kwa Wananchi ili kuboresha  maisha  yao ifikapo mwaka 2020.

Ili kutekeleza kwa ufanisi  yale yote  yaliyoainishwa katika Mpango Mkakati wetu, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti  imeweka  Mikakati itakayohakikisha  kwamba  kwa kutumia  fursa  na Rasilimali zilizopo, malengo tuliyojiwekea  yanafikiwa. Mkataba wa Huduma kwa mteja ni moja ya Mkakati muhimu.

Katika Mkataba huu, tumewaonesha  Wateja wetu, Huduma  tunazotoa na Viwango vya Huduma  Mteja  atakazopokea. Aidha, tumeonyesha Haki na Wajibu wa Wateja wetu. Utaratibu wa kupokea  na kushughulikia Malalamiko na taratibu za Rufaa pale  ambapo  Mteja wetu hataridhika  na Huduma aliyopewa.

Kwa Madhumuni ya Mkataba huu Wateja  wetu ni wa aina mbili:-

  • Wateja  kutoka ndani ya  Taasisi (Watumishi wa Umma)
  • Wateja kutoka  nje  ya Taasisi (Wakazi  wa Wilaya ya Serengeti na nje ya  Wilaya)

Matarajio yetu ni kwamba Mkataba huu utatuweka karibu na Wateja wetu, na kutoa  fursa nzuri kufahamu kwa hakika mahitaji halisi ya  Wateja  wetu na kusaidia  kubuni mbinu sahihi za  kukabiliana na  changamoto zitakazojitokeza.

Wateja wetu mnaombwa na kukaribishwa  kuendelea  kutumia  huduma zetu. Zaidi mnaombwa kutoa ushauri na mapendekezo pale ambapo  mtaona  kunahitaji marekebisho.



Eng. Juma Hamsini

MKURUGENZI MTENDAJI (W)

SERENGETI

 

 

  • MADHUMUNI YA MKATABA HUU:-

Madhumuni ya Mkataba huu  ni kuweka  mfumo unaokubalika  pande zote  mbili, mtoaji na mpokea huduma kwa nia  ya kuimairisha  ari ya  uelewano na  kuainisha Ubora wa Huduma na hali ya  kuwajibika kwa pande zote.

Mkataba huu unawapa Wateja wetu fursa ya kuzifahamu kinagaubaga Huduma tunazozitoa na Viwango vya Huduma  zinazotolewa. Aidha, Mkataba huu unamfahamisha  Mteja  wetu juu ya  Haki na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko endapo hataridhika na Huduma zetu au kuwasilisha  changamoto/mawazo mapya kwa nia ya  kuboresha  Huduma zetu.

  • MAJUKUMU NA WAJIBU WETU:-

Majukumu na Wajibu  wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti  yameinishwa  katika Sheria ya Serikali za Mitaa ( Mamlaka za Wilaya Na.7) ya Mwaka 1982. Majukumu na Wajibu huu upo katika maeneo yafuatayo:-

2.1 Wajibu wa Kiutawala:

Wajibu  huu unalenga katika kuhakikisha  kwamba  kunakuwepo na  Amani, Usalama na Upendo kwa wakazi wote. Aidha ni  wajibu wa kiutawala wa Halmashauri kuzisaidia Halmashauri za Vijiji na Vitongoji  katika eneo lake kwa kuziwekea  mfumo na Mazingira mazuri ya kutekeleza majukumu yake kwa  kufuata Misingi na Kanuni za Utawala Bora.

  • Wajibu wa Kimaendeleo:

2.2.1 Kiuchumi:

  • Ni jukumu la Halmashauri kupitia Wataalam wake wa Sekta, kubuni Mipango na Mikakati itakayowezesha Mteja mmoja mmoja au katika vikundi kutumia Rasilimali zilizopo kuborsha hali zao za maisha kwa kuwajengea  uwezo katika  shughuli zao za  uzalishaji mali kwa lengo la kujiimarisha  huku wakizingatia zana ya Maendeleo endelevu.
  • Kijamii:
  • Ni jukumu la Halmashauri  kupitia Wataalamu wake wa  Kisekta, kubuni Mipango na Mikakati itakayo mwezesha  Mteja  mmoja mmoja  au  katika Vikundi kupata Huduma za Kijamii (Huduma muhimu kwa mtu kuishi) kwa wakati na kwa usawa bila kujali tofauti za Watu katika vipato.
  • Wajibu wa uwakilishi:
  •  

2.3.1 Kisera:

  • Ni wajibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kupeleka na kusimamia Sera, Sheria, Maagizo na Mipango ya Serikali Kuu kwa Wananchi katika maeneo yao, na kuhakikisha  utekelezaji wake. Jukumu hili linaiwajibisha Halmashauri kuhakikisha kila Mwananchi kuhisi uwepo wa Serikali na kila mahali alipo, na  kumuwezesha kufanya kazi zake  vizuri bila kuvunja Sheria.
  • Kidemokrasia:
  • Ni wajibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kuhakikisha kuwa Demokrasia na Utawala Bora katika uendeshaji na Usimamizi wa shuguli za Watu na Maendeleo yao vinatekelezwa kwa kiwango kinachokubalika. Kila Taasisi za Serikali za Mitaa ndani ya Halmashauri ya Wilaya iongozwe kwa Maamuzi ya Wananchi, aidha kupitia Wawakilishi wao au wenyewe.
  •  
  • MISINGI YA UTOAJI HUDUMA  KWA UMMA.
  • Kujiwekea Viwango vya Huduma.
  • Tutaweka  viwango vilivyo bayana  vya Huduma  ambavyo Wateja wetu watavitarajia kuvifuatilia na kupima matokeo.
  • Kufanya kazi kwa  uwazi:
  • Katika kutekeleza Majukumu yetu kwa Mteja, tutajizatiti kuzingatia zana ya  uwazi. Tutakuwa tayari kutoa Taarifa zote ambazo kwa mujibu wa Mkataba huu na Sheria na  Kanuni nyingine Mteja wetu anayo haki ya  kuzipata. Aidha, mawasiliano yetu na  Wateja  wetu  yatakuwa katika Lugha na mfumo  rahisi ambao unaeleweka kwa aina zote za Wateja wetu.
  • Ushirikishwaji:
  • Ili kuweka Huduma zetu katika ubora unaohitajika na Wateja, suala la  kuomba  ushauri na kushirikisha Wateja wetu katika kutoa mawazo, mapendekezo na dukuduku zao katika  maeneo mabalimbali  ya utedaji wetu litapewa  kipaumbele. Tumaini kwa kufanya hivyo muda wote tutakuwa sawia na mahitaji ya wateja  wetu.
  • Kutenda Haki:
  • Huduma zetu zitamlenga Mwananchi na Watu wote. Tunatambua uwepo wa tofauti nyingi miongoni mwa Wateja wetu kwa misingi ya itikadi za Kisiasa na Dini, Kijinsia, Kijiografia, Kiuchumi, Kielimu, Kikabila na Kimaumbile. Huduma zetu zitawalenga Wateja wote bila  kujali kundi lolote la Kijamii Mteja wetu alimo.
  • Kutoa Huduma kwa Ubora wa Juu:
  • Tutajitahidi kuona kwamba pamoja  na Huduma zetu kutolewa  kwa wakati, pia ubora wake upo katika kiwango kinachokubalika. Tutajitahidi kutumia Teknolojia ya Kisasa na kuwapa Wateja wetu Huduma nzuri na ya haraka.
  • Kushughulikia Migogoro/Matatizo yanayojitokeza:
  • Wakati wote, Lengo letu katika kushughulikia mogogoro/Matatizo itakuwa ni  kuhakikisha kwamba ufumbuzi  unapatikana haraka kwa nia ya kupunguza madhara ya  Migogoro hiyo na Wateja wetu wnapewa taarifa mapema jinsi ilivyoshughulikiwa. Tuatajizatiti muda wote kupitia taratibu zetu za  kushughulikia Kero kwa nia ya kuziborsha.
  • Matumizi Bora ya Rasilimali tulizonazo:
  • Tutatumia Rasilimali zote tulizonazo kwa makini na uangalifu mkubwa kwa Masilahi ya Ustawi wa Taasisi hii na Wateja wake. Tutasisitiza usawa katika matumizi ya Rasilimali. Aidha, pale inapobidi kugawana Rasilimali hizo; Sheria, Kanuni na Taratibu zinazohusika zitatumika.
  • Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
  • Kama ilivyotamkwa katika Sera ya Taifa juu ya uendeshaji wa Bajeti inayojali Matokeo (Perfomance Budget) Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti itakuwa ni ile inayojali Matokeo (Output to Input Budget and not Input to Out Budget). Hivyo Budget itakuwa  ni chombo cha Menejimenti na sio  Wahasibu  na kila Wakuu wa Idara  atawajibika na utekelezaji usioridhisha  wa Bajeti ya Idara  yake bila kuwasingizia Wahasibu. Wahasibu na Mweka Hazina watakuwa  washauri tu juu ya ufuatiliaji wa Taratibu na Kanuni za Matumizi ya Fedha za  Serikali na sio waamuzi.
  • Rasilimali Watu:
  • Uendeshaji wa Rasilimali Watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti unaozingatia matokeo (Result Oriented Management) kama ilivyoainishwa kwenye Sheria Na.8 ya Utumishi wa Umma (2002), Kifungu Na.6 (a), kila Mtumishi atapimwa  Utendaji kazi wake  kwa kuzingatia  hali halisi  ya utendaji kazi wake kwa kurejea kwenye mpango Mkakati wa Halmashauri ya Wilaya uliopo.
  • Ushirikiano wa Watoa Huduma wengine:
  • Muda wote tutaheshimu na kuthamini mchango unaotolewa  na watoa Huduma wengine  katika Wilaya. Tutahakikisha  tunawapa Ushirikiano na Msaada kila wanapohitaji.
  • WATEJA WETU.
  • Mpango mkakati kati ya Halmashauri (Medium Term Strategic Plan 2008 – 2011 imeainisha Wateja wetu kama ifuatavyo:-
  • Mwanachi.
  • Kupata ufumbuzi/ufafanuzi wa shida yake/zake kwa wakati
  • Kupata  ushauri
  • Kuwekewa Mazingira mazuri ya kufanya  shughuli zake
  • Kuunganishwa na watu/vikundi mbalimbali kwa ajili ya  kukuza  ujuzi katika  shughuli zake.
  • Kupata Utaalamu mbalimbali.
  • Mtumishi.
  • Kuendelezwa Kiutumishi
  • Kupata  Ujira wake anastahili kwa wakati
  • Kupata  stahili zake za  Kiutumishi
  • Kutenda kazi kwa  kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya kazi.
  • Kutekeleza Majukumu na Maagizo kama atakavyoelekezwa /kuagizwa  na viongozi wake wa kazi.
  • Serikali za Vijiji/Viongozi.
  • Kupata  Ushauri
  • Kupata Msaada wa tafsiri za Sera, Miongozo na Sheria mbalimbali
  • Kupata  Msaada wa Rasilimali.
  • Mashirika ya Dini, NGO’S na Taasisi za Kiraia.
  • Kupata msaada wa Wataalamu
  • Kupewa maelezo mbalimbali na maeneo wanayofanyia kazi
  • Kupata Taarifa  na Takwimu kwa ajili ya  matumizi ya Ofisi zao.
  • Kuunganishwa  na wananchi/Serikali za vijiji.
  • Wizara, Sekretarieti na Wakala wa Serikali.
  • Kupewa Taarifa/Ripoti sahihi kwa wakati
  • Kutekeleza Mipango ya Wizara/Wakala wa Serikali katika ngazi za chini
  • Kupata Taarifa  za Utekelezaji wa Sera na Mipango katika ngazi za vijiji na kaya
  • Kusaidia kukusanya  Takwimu, Mapendekezo na maoni ya wnanchi.
  • Wahisani.
  • Kuwapatia Taarifa na Ripoti Sahihi
  • Kuwezesha Usalama na Utulivu kwao
  • Kuwezesha kuwepo kwa Uwazi katika utendaji wao wa kazi
  • Kuwaandalia Mipango mizuri ya utendaji kazi.
  • Kuwapatia Taarifa sahihi ya Matumizi ya Fedha.
  • Wanasiasa.
  • Kutofungamana na upande wowote ( Political Impartiality)
  • Kuwapatia Taarifa sahihi za  utekelezaji wa Ilani
  • Kuwapatia Taarifa na Kumbukumbu sahihi kuhusu shuguli za Uchaguzi.
  • Jumuiya za Wafanyakazi
  • Kufanyiwa Malipo kwa wakati
  • Kushughulikiwa shida zao kwa wakati
  • Vyombo vya Habari.
  • Kutoa habari inayoombwa.
  • Kuwapa  ushirikiano unaostahili.
  • MAADILI KATIKA  KUTEKELEZA MAJUKUMU YETU.
  • Katika kuwahudumia  wateja wetu na kutekeleza tuliyoyaainisha katika  Mkataba huu, Watumishi wote  tutaongozwa na kuzingatia maadili na miiko ya Taaluma zetu ya kazi katika  Utumishi wa Umma, kama yaliyoainishwa  katika Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003, Kanuni Na. 65 za Sheria  Na. 8 ya Utumishi wa UMMA, 2002.
  • UBORA WA VIWANGO  VYA UTENDEJI KAZI KWA  WATEJA
  • Muda wote tutajitahidi kutoa huduma zetu kwa wateja wetu huku tukitoa kipaumbele katika maeneo muhimu ya matokeo kama ifuatavyo:-
  • Kutoa Huduma kwa wakati.
  • Katika kumhudumia mteja wetu, suala la wakati litapewa  kipaumbele. Tutajizatiti kuona kwamba, kama mteja wetu atakuwa  ametimiza wajibu wake kama ulivyoelezwa katika Mkataba  huu, anapokea Huduma ndani ya muda uliokubalika.
  • Kutoa Huduma yenye Ubora (Quality)
  • Tutakuwa  makini muda wote  kuhakikisha  Huduma zetu ni za  kiwango cha juu na kinakidhi mahitaji ya wateja wetu.
  • Kutoa Huduma kwa kiasi kinachotarajiwa.
  • Pamoja na  masisitizo katika kutoa huduma kwa wakati na ubora, pia tutajizatiti kutoa Huduma (Tangable Service) kwa  kiasi kinachotakiwa kulingana na  rasilimali zitakazokuwepo.
  • HAKI YA MTEJA WETU.
  • Katika  Mkataba huu, Mteja anayohaki ya kupokea Huduma ya kiwango cha juu kutoka kwetu. Aidha, pamoja na haki hiyo, Mteja wetu atakuwa  na haki zifuatazo;-
  • Haki ya kupokelewa katika Ofisi na kusikilizwa  kwa heshima.
  • Haki ya kushiriki katika majadiliano yanayohusu masuala ambayo Mteja ana Maslahi na kwa Mujibu wa sheria  anayohaki ya kushiriki.
  • Haki ya faragha na kutunza Siri.
  • Haki ya kukata Rufaa au kutafuta Huduma pengine endapo hataridhika na Huduma  aliyopata.
  • WAJIBU WA MTEJA WETU.
  • Tunaamini  ili Mteja wetu aweze kupata Huduma nzuri, hana budi kuwa  ametimiza wajibu wake  ambao utakuwa unaambatana na Huduma anayoitafuta kwetu.
  • Kwa mantiki hiyo Mteja wetu atakuwa na wajibu ufuatao:-
  • Kutoa maelezo /Taarifa iliyosahihi na kwa wakati
  • Kufuata Taratibu, Sheria na Kanuni.
  • Kufika Ofisini au mahali anapotakiwa  kufika kwa wakati.
  • Kuwa na uhusiano mzuri na Watumishi.
  • Kusikiliza kwa makini maelezo anayopokea kutoka kwa Afisa  na inapobidi maelezo hayo kutolewa kwa Mamlaka nyingine afanye hivyo kupoteza  usia wake.
  • MUDA WA KUTOA HUDUMA KWA MTEJA (RATIBA)

Tutashughulikia hoja za wateja wetu mapema  na kutoa huduma  haraka iwezekanavyoz:-

NA.

HUDUMA

MUDA/SIKU

1.
Kutoa Ushauri na Huduma za Kitaalamu kwa Wakulima na Wafugaji na Wananchi
Siku 7 baada ya hitaji kujitokeza
2.
Kupeleka matokeao ya Utafiti mbalimbali kwa wakulima na  wafugaji
Siku 7 baada ya hitaji kujitokeza
3.
Kutoa Huduma ya Tiba  /chanjo kwa magonjwa ya mlipuko ya mifugo na mimea
Siku 2 baada ya kupokea taarifa
4.
Kutoa  mafunzo ya uendeshaji mifugo na kilimo Bora
Siku 14 baada ya fedha  kupatikana kutegemeana na  msimu
5.
Kutoa Taarifa za Utekelezaji kwa Mamlaka mbalimbali
Siku 10 baada ya kipindi cha kutoa  Taarifa husika  kuisha.
6.
Kutoa Elimu kwa Watumishi kuhusu badiliko lolote katik Utumishi.
Siku 7 baada ya kupokea badiliko.
7.
Kukiri kupokea  kwa barua/ombi  n.k.
Siku 2
8.
Faili la Mteja  au linalohusu Huduma yoyote itolewayo na Halmashauri litakaa kwa Mkuu wa IDARA ILE
Siku 14 tu, baada ya  hapo liwe  limepelekwa  hatua ya mbele  ya utekelezaji. Register ya mzunguzo wa mafaili itaonesha  Mkuu wa Idara atakae kuwa   amekaa na  Faili nje ya  muda husika na Mwangalizi wa Ofisi atatoa taarifa kuhusu uchelewesha  huo kwa Mkurugenzi  kila siku Asubuhi kwa hatua zake, na Mkuu wa Idara anatake  chelewesha zaidi ya mafaili saba ndani ya wiki moja  atatolewa  Taarifa  kwa Mamlaka ya  Nidhamu (Halmshauri ya Wilaya)
9.
Upandishaji vyeo watumishi waloidhinishwa kwenye bajeti  ya mishahara kwa mwaka  - mwezi 1tangu kwanza  kwa mwaka wa fedha

10.
Kurekebisha  mishahara  ya watumishi waliopandishwa  cheo
Siku 30 baada ya mwajiri kuidhinisha  na mtumishi kukubali cheo hicho.
11.
Kushughulikia maslahi/malipo ya wafanyakazi
Siku 30 baada ya kupanda cheo
12.
Kutuma nyaraka  zinazohusu mafao ya Hitimisho la kazi; Pensheni na Mirathi Makao MAKUU
Miezi 6 kabla ya mtumishi kupata sifa za kulipwa mafao ya kustaafu.
13.
Kushughulikia Arrears za Watumishi
Siku 30
14.
Kutoa mafunzo kwa Watumisi
Siku 14 baada ya  Taarifa kupokelewa
15.
Malipo kwa Wazabuni
Siku 14 baada ya  kazi kukamilika
16.
Kushughulikia Nidhamu za Watumishi ( Makosa madogo
Siku 14 baada ya kupokea taarifa.
17.
Kuthibitisha Watumishi kazini
Siku 60 baada ya  kumaliza kipindi cha majaribio.
18.
Kushughulikia Ajira
Siku 60 baada ya kutoa tangazo la Ajira
19.
Kufanya  Tathimini ya Utendaji kazi (OPRAS)
Siku 7 za mwanzo za mwezi Julai.
20.
Kushughulikia  na kutatua  migogoro ya uongozi katika  serikali za  Vijiji.
Siku 30 baada ya  Taarifa kupokelewa za mgogoro
21.
 Kujaza nafasi wazi katika serikali za vijiji na vitongoji
Siku 90
22.
 Kutoa ushauri wa kisheria kwa mapendekezo ya Rasimu ya sheria  ndogo za vijiji.
Siku 30 baada ya maoni kutoka serikali ya Kijiji
23.
Kutoa majibu kwa malalamiko ya wananchi dhidi ya  HALMASHAURI (CMT) na kamati ya fedha, uongozi na mipango
Siku 14 baada ya Taarifa ya Ukaguzi kutolewa.
24.
Kutoa Ripoti  ya uchaguzi maalum  special check and Investigations) kwa Mkurugenzi Mtendaji (w)
Siku 7
25.
Kuandikisha chama cha   Akiba  na Mikopo (SACCOS)
Siku 30 baada ya Mkutano Mkuu uanzilishi.
26.
Kuanzisha vyama vingine
Siku 60
27.
Kufanya  Usuluhishi wa mgogoro katika chama
Siku 60 baada ya  kupokea  Taarifa  za mgogoro
28.
Kufanya  Ukaguzi wa chama cha Msingi  na kutoa  Ripoti
Siku 20 tangu kwanza Ukaguzi
29.
Kupitisha  Makisio, Maoni na Nyaraka za CHAMA
Siku 2
30.
Kufanya usajili wa Walimu wapya
Siku 90.
32
31.
Kufanya  Ukaguzi  na kutoa Taarifa ya Ukaguzi kwa Wadau
Siku 14 baada ya  kumaliza Ukaguzi.
32.
Kufanya Semina  na Warsha za Mada Ngumu/Tata
Siku 14 baada ya Fedha kutolewa/kupatikana
33.
Kuandikisha Watoto Darasa la Kwanza
Siku 30 kabla ya  kwanza Muhula wa I
34.
Kuandaa na Kusimamia  Mitihani ya Muhula wa I na II
Siku 30 kabla  tarehe ya  kumaliza  Mitihani ya Darasa la  IV.
35.
Kufanya maandalizi  na kuendesha Mtihani wa Taifa wa Darasa la  IV na VII.
Siku 30.
36.
Kuchagua  Wanafunzi wa kuingia Kidato cha I
Siku 21 baada ya Matokeo ya Darasa la saba.
37.
Kufanya  Ukaguzi na kutoa  Ripoti ya Miradi ya MMEM kwa Wadau
Siku 14 baada ya  Ukaguzi .
38.
Kutoa Mikopo kwa Vikundi vya Uchumi/Ujasiriamali
Siku 10
39.
Kufanya Uhamasishaji na kuandaa vikundi vya  Uchumi/Ujasiriamali hadi hatua ya  kusajiliwa /kupewa  mkopo.
Siku 60.
40.
Kutoa huduma  ya maji kwa mteja nyumbani
Siku 2 baada ya  kupokea maombi.
41.
Kufanya utafiti wa chanzo cha  maji na kutoa matokeo
Siku 3 baada ya  kupokea ombi
42.
Kuchimba Visima virefu vya maji- Miezi 4 (Visima vifupi
Siku 14
43.
Kuchimba Malambo
Siku 90
44.
Kufanya  Ukarabati wa Miundo Mbinu na Maji
 Siku 1 baada ya  kupokea  Taarifa.
45.
Kuanzisha na Kusajili Juimuya za watumia maji – miezi 6 baada ya  kuandaliwa/kupatikana  kwa Rasimu

46.
Kutoa Leseni ya Biashara
Siku 3
47.
Kutoa Elimu na Ushauri kwa  wananchi juu ya Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji wa Biashara
Siku 14 baada ya fedha kupatikana.
48.
Kukagua vitabu vya Mapato  nyumba za  kulala wageni
Siku 7 za mwanzo kila mwezi.
49.
Kutoa Taaarifa ya Maduhuli Wizara ya Ardhi na Maendeleo  ya Makazi.
Siku 14.
50.
Kushughulikia mgogoro wa Ardhi ( mashamba)
Siku 14
51.
Kushughulikia mgogoro wa mipaka ya vijiji
Siku 7
52.
Kushughulikia mgogoro wa Mipaka Wilaya /Mkoa
Siu 7
53.
Kutaifisha kiwanja ambacho kimetolewa Notisi na muda wa Notisi umekwisha ambacho hakijaendelezwa
Siku 7
54.
Kufanya  Ukaguzi wa majengo ambayo hayajafuata Taratibu za Mpango  Mji na kutoa Taarifa.
Siku 2 baada ya  Ukaguzi.
55.
Kutoa majibu ya maombi ya kiwanja miezi 6

56.
Kutoa Leseni za uvunaji wa mazao ya  misitu na  nyuki
Siku 90
57.
Kutoa Leseni za  Uwindaji
Siku 1
58.
Kutoa Elimu kuhusu matumizi ya masharti mbadala
Siku 3 baada ya  Mtoaji
59.
Kufanya Maandalizi ya siku ya kupanda  miti
Siku 7
60.
Kushughulikia  matukio ya wanyamapori walioshambulia mashamba na makazi
Siku 1
61.
Kuitikia Taarifa za Ujangiri
Siku 1
62.
Kutoa Hati ya kumiliki nyaraka
Siku 2
63.
Kuondoa makundi ya  nyuki wasumbufu kwenye  makazi ya  watu.
Siku 1
64.
Kutoa Kibali cha kwanza kujenga nyumba baada ya  ombi la  kutolewa
Siku 7
65.
Kulipa Fidia ya Ardhi
Siku 90 tangu Ardhi kutawaliwa
66.
Kutoa barua ya Toleo (Letter of Officer)
Siku 90
67.
Kupima Viwanka  katika Taasisi, Shule, Makanisa n.k.
Siku 7 baada ya ombi kupokelewa.
68.
Kurudishia alama za Viwanja (Beacons)
Siku 3 baada ya ombi kupokelewa
69.
Kutoa Taarifa ya Orodha ya Dawa zilizopo Hospitali
Siku 3
70.
Kutoa taarifa Huduma ya chanjo za Kliniki za Mkoa (Mobile) mara 1 kila mwezi kwa maeneo ambayo hayana  zahanati.

71.
Kutoa Huduma ya chanjo kwenye  vituo vya Afya/Zahanati
Kila siku ya kazi

DAMPO LINAPOJAA

72.
Kufanya ukaguzi wa mazingira mara kwa mara
Siku 30
73.
Daktari kuona wagonjwa (Ward round) waliolazwa Wadoni
Kila siku asubuhi.
74.
Kufanya uchuguzi/vipimo na kupewa matokeo

  • B/S Dakika 30
  • Window Test Dakika 120
  • Mokotaozi – saa 24
  • X – ray Dakika – 45
  • Utra – sound Dakika 60
  • Kutoa Huduma ya Afya ya uzazi na mtoto
  • - Hudhurio la kwanza – dakika 60
  • - Hudhuri la marudio – dakika 30
  • Kupokea Huduma dirias la kupokea Dawa – Dakika 10
  • Kufanya Ziara za Usimamizi (Supportive Supervision) katika Vituo vya Afya na Zahanati – siku 15 baada ya Robo mwaka kuisha.
  • Kutoa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto – kufuatana na Tarehe aliyopangiwa saa moja tangu kufika Kliniki.
  • Maombi ya Fedha kwa Mteja kulipa ndani ya  siku nne kama ifuatavyo:-
  • Fomu ya maombi kushughulikiwa na  kuwa imesainiwa na Mkuu wa Idara  husika, Mweka Hazina na Mkurugenzi Mtendaji (W) siku mbili.
  • Kuandikwa vocha na cheki na kuwa  vimekamilika kusainiwa siku mbili.
  • Ikiwa kuna matatizo yoyote katika maombi ya fedha ya mteja  atajulishwa kwa barua baada ya siku mbili tangu kuwasilisha  kwa maombi hayo. Na sio kusubiri mteja kufuatilia.
  • Ili kuwezesha hili, Regista maalum kuonesha mzunguko wa barua  itaanzishwa ili kubaini nani anakwamisha  huduma bora na kwa wakati mteja wetu.
  • MIADI:
  • Wakati wote, lengo letu litakuwa kumhudumia mteja wetu haraka  iwezekanavyo. Inapobidi kutoa miadi, tutajitahidi miadi yote ifanyike ndani ya Dakika 30 tangu muda wa hundi kutimia.
  • UTARATIBU WA KUPOKEA MALALAMIKO/MIGOGORO.

Tutakaribisha maoni kuhusu Mkataba wetu wa Huduma kwa Mteja au malalamiko kuhusu Huduma zetu. Mteja wetu anaweza kuwasilisha Maoni/Malalamiko yake kwa kutumia moja wapo ya njia tulizozielekeza hapo chini:-

  • Kuonana na Afisa ana kwa ana.
  • Mteja atafika Ofisi za Halmashaui sehemu ya Mapokezi ambayo itaandaliwa katika kila Idara kuelekezwa kwa Afisa anayehusika.
  • Visanduku vya Maoni:
  • Mteja wetu atatumbukiza lalamiko lake katika visanduku vya maoni vilivyowekwa katika Ofisi za Halmashauri, Hospitali, Zahanati, Mashuleni Ofisi za Watendaji wa Kata na Vijiji.
  • Vikao vya Serikali ya Kijiji.
  • Mteja wetu anaweza kupitisha lalamiko lake katika vikao vya serikali za vijiji na Kata hatimaye kuwekwa kwenye Kumbukumbu za Halmashauri za Wilaya.
  • Posta, Simu, Fax na Barua pepe.
  • Mteja anaweza kutuma lalamiko kwa kutumia Anuani
  •  
  • Dawati la Kero/Malalamiko 
  • Dawati hili lipo Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti hupokea huratibu na kushughulikia malalamiko muda wote wa saa za kazi.
  • Mkurugenzi Mtendaji (W),
  • Halmashauri ya Wilaya Serengeti
  • S.L.P.344,
  • Mugumu/Serengeti
  •  
  • Simu Na………………..
  • Fax Na…………………..
  • UTARATIBU WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO.
  • Tungependa kuwa na Mfumo wa kushughulikia malalamiko wenye ufanisi na manufaa zaidi kadri inavyowezekana. Hivyo tungependa mfumo ufuatao wa kushughulikia malalamiko utumike.
    • Lalamiko dhidi ya 
    • Liwasilishwe kwa
    • Mkuu wa Idara
    • Mkurugenzi Mtendaji (W)
    • Mtumishi
    • Afisa Utumishi (W) au Mkuu wa Idara
    • Mkurugenzi Mtendaji (W)
    • Katibu Mkuu - TAMISEMI

    • UTARATIBU WA KUTOA MREJESHO
    • Wateja wetu ambao Anuani zao siyo bayana, itawapa kuacha Ofisini utaratibu ambao Ofisi itautumia kuwafahamisha matokeo/maendeleo ya utatuzi wa masuala yao
    • KUKATA RUFAA.
    • Kama ambavyo tumetaja awali, Rufaa ni Haki ya Mteja wetu iwapo ataona Huduma yetu haijamridhisha. Kwa Mantiki hiyo, Mteja wetu atakuwa huru kukata Rufaa kwa Mamlaka ya juu au kutafuta ufumbuzi katika vyombo vingine nje ya mfumo huu. Mfumo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambayo anuani yake ni :
  •  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,


    •  S.L.P.2643,
    •  Dar es salaam,
    •  Tanzania.
    •  Simu Na. 002 – 2110607
    •  
    • Tume ya Utumishi wa Umma,
    • Jengo la Ubungo Plaza
    • Gorofa ya nane
    • Barabara ya Morogoro
    • S.L.P.9143,
    • Dar es salaam,
    •  
    • Tanzania – Inapombidi Mteja wetu kufanya hivyo, ni muhimu atupatie Taarifa  na nakala yake ya Rufaa
    • MAPITIO YA  MKATABA HUU:
    • Tunaamini kwamba Mkataba huu umejumuisha maeneo yote muhimu yanayogusa hali halisi ya maisha wa wateja wetu wote kwa kutilia maanani Mazingira halisi tunayoishi.
    • Hivyo tunaamini ili Mkataba huu uendelee kuyagusa maisha  halisi ya  Mteja wake.
    • Unahitajika kufanyiwa Mapitio/Tathimini  mara kwa mara kwa nia ya:-
    •  Kuufanya Mkataba huu uweze kuwa sambamba  na mabadiliko  
  •    muhimu yanayojitokeza katika Jamii.


    •  Kubaini Dosari/Mapungufu yaliyo jitokeza katika kipindi cha
  •    Utekelezaji wake.


    • Kubaini iwapo Mkataba huu  bado unakidhi Msingi ya Huduma kwa Wateja
    • Kujua iwapo Viwanjo na Malengo tuliyowekea yanakwenda sambasamba na mhitaji na matarajio ya wateja wetu.
    • Kujua kama mambo yaliyomo katika Mkataba huu bado ni sahihi.
    • USHAURI KATIKA MAPITIO
    • Ili tuweze kutimiza tulio waahidi wateja wetu, tunakaribisha Ushauri, Maoni Changamoto, zozote kutoka kwa wateja wetu.
    • Tutatumia Sherehe za Sikuu ya Serikali za Mitaa, (1 Julai) kila mwaka tulivyotekeleza ahadi zetu kulingana na malengo tuliyojiwekea.
    • Tutatoa maendeleo ya utendaji ya ahadi zetu kwa wateja.
    • Tutatoa maendeleo maendeleo ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja kwa wadau wetu wote.
    • Tutatoa taarifa kuhusu malalamiko tuliyopokea na jinsi tulivyoshughulikiwa. Ardhi, tutatumia muda huu kupokea maoni kwa wateja wetu maoni tutakayotumia kuborsha Mkataba.
    • MAHALI TULIPO NA MUDA WA KAZI.
    • Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti zipo Mugumu Mjini.
    • Karibu na Benki ya - NMB

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA 2023 December 13, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA YA UELIMISHAJI RIKA JUU YA VVU NA UKIMWI November 11, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 28, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 04, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MADIWANI WAIOMBA TANAPA KUGUSA KATA ZOTE SERENGETI KIUWEKEZAJI

    March 02, 2023
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA PILI 2023

    February 28, 2023
  • ZAIDI YA BILIONI 14.268 KUTUMIKA KUTENGENEZA BARABARA SERENGETI

    March 02, 2023
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI, NA MIPANGO IMETEMBELEA NA KUKAGUA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA SEKONDARI NYICHOKA

    February 18, 2023
  • Angalia zote

Video

DKT.MASHINJI ASITISH A SHUGHULIZA UCHIMBAJI KOKOTO KUFUATIA KIFO CHA MCHIMBAJI
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti