• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Idara ya Ardhi na Maliasili


Idara hii Imegawanyika katika sekta mbili (2) ambazo ni sekta ya ardhi na sekta ya maliasili.

  • Sekta ya Ardhi - Imegawanyika katika sehemu nne (4) ambazo ni uthamini, mipango miji, upimaji na ramani na Ardhi utawala na usimamizi.
  • Sekta ya Maliasili – Ina sehemu mbili (2) ambazo ni misitu na wanyamapori 

Majukumu ya Idara ya Ardhi na Maliasili

Majukumu ya idara ya ardhi na maliasili kwa kuzingatia sehemu ya uthamini, mipango miji, upimaji na ramani, ardhi utawala na usimamizi, misitu na wanyamapori ni kama ifuatavyo:

Sehemu ya Uthamini

Majukumu ya mthamini ni:

  • Kukusanya taarifa za utafiti na mwenendo wa soko la ardhi
  • Kuhakiki kumbukumbu za utafiti na kuziingiza kwenye komputa
  • Kupokea maombi na kufanya uthamini wa ardhi, mazao,majengo na samani
  • Kukagua, kupima na kuoanisha thamani ya majengo na ardhi kwa ajili ya kumbukumbu
  • Kukadiria kodi ya ardhi

Sehemu ya Mipango miji

Majukumu ya Afisa mipango miji ni:

  • Kuandaa mipango ya maeneo yaliyoendelezwa kiholela/ urasimishaji wa makazi holela
  • Kuandaa michoro ya mipango miji kwa maeneo ambayo hajaendelezwa
  • Kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji
  • Kuchambua takwimu na taarifa kwa ajili ya maandalizi ya mipango mipya ya makazi
  • Kupokea michoro ya mipango miji na taarifa za maeneo ya ardhi yanayopendekezwa kuiva kwa ajili ya uendelezaji kimji
  • Kupokea na kuweka kumbukumbu za maombi ya mabadiliko ya matumizi na umegaji wa viwanja
  • Kuhakikisha kuwa mabadiliko ya matumizi ya ardhi yanaingizwa katika michoro

Sehemu ya Upimaji na Ramani.

Upimaji na ramani ni miongoni mwa vitengo vingine vya ardhi kama vile, utawala na usajili ardhi, uthamini pamoja mipango miji kitengo hiki kina majukumu mbalimbali ndani jamii katika kutoa huduma zake.

Majukumu ni kama vile upimaji wa viwanja, upimaji mashamba, kuonyesha mipaka ya viwanja na mashamba, kutatua mogogoro ya ardhi, kutoa elimu ya ardhi kwa wananchi.

Sehemu ya Ardhi Utawala na Usimamizi.

Majukumu ya Afisa Ardhi ni kama ifuatavyo:

  • Kupokea maombi yanayohusu Hati miliki na kutunza usajili wa maombi husika
  • Kushughulikia utayarishaji wa nyaraka za kisheria
  • Kutoa notisi na kupendekeza ubatilishaji wa miliki za viwanja visivyoendelezwa kwa mujibu wa sheria
  • Kuwasiliana na wateja kuhusu Hati zilizotayarishwa na kuwakabidhi
  • Kutoa ushauri na mapendekezo ya ugawaji wa viwanja na mashamba
  • Kufanya ukaguzi wa viwanja

Sehemu ya misitu

Majukumu ya afisa misitu ni kama ifuatavyo:

  • Kutoa elimu ya Hifadhi ya Mazingira, kuhimiza uoteshaji miche ya miti na upandaji miti
  • Kutoa elimu juu ya utengaji wa misitu ya asili (ngitiri) na utunzaji wa misitu ya asili (ngitiri)
  • Kusimamia hifadhi ya wanyamapori na hifadhi za misitu
  • Kutoa elimu ya hifadhi ya mazingira ,ardhi na vyanzo vya maji.

Sehemu ya wanyamapori

Majukumu ya afisa wanyamapori ni:

  • Kuthibiti utoaji wa leseni za biashara ya nyara na vibali vya kukamata wanyamapori
  • Kuthibiti matumizi haramu ya leseni za uwindaji na kuhakikisha kufuatwa kwa maadili katika kutumia wanyamapori
  • Kushiriki katika kusuluhisha migogoro ya matumizi ya wanyamapori
  • Kuthibiti matumizi haramu ya wanyamapori
  • Kufanya kazi za kuzuia ujangili
  • Kufuatilia utekelezaji wa miongozo mbalimbali ya uhifadhi wa wanyamapori
  • Kukusanya taarifa na takwimu za uhifadhi wanyamapori
  •  Huduma za jamii zinazotolewa
  • Kurasimisha  makazi holela
  • Kuandaa michoro ya mipango miji kwa maeneo ambayo hajaendelezwa
  • Kuwasiliana na wateja kuhusu Hati zilizotayarishwa na kuwakabidhi

Kazi za Jumla katika Idara ya Ardhi na Maliasili

  • Kuratibu na kudhibiti uendelezaji wa Miji na Vijiji.
  • Kuratibu uandaaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi Vijijini na Mijini.
  • Kujenga uwezo wa kupanga na kutekeleza majukumu ya uendelezaji ardhi kwenye Halmashauri.
  • Kuelimisha jamii kuhusu Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi.
  • Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Ardhi.
  • Kubaini fursa na vikwazo vya uendelezaji.
  • Kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa mipango ya Miji na Vijiji inayoandaliwa.
  • Kusimamia uendelezaji wa maeneo ya makazi.
  • Kushughulikia maombi ya mabadiliko ya matumizi ya kiwanja, muunganiko/mgawanyo wa kiwanja.
  • Kukusanya taarifa za utafiti na mwenendo wa soko la Ardhi.
  • Kuhakiki kumbukumbu za utafiti na kuziingiza kwenye kompyuta
  • Kupokea maombi na kufanya uthamini chini ya usimamizi wa Mthamini aliyesajiliwa
  • kukagua, kupima na kuoanisha thamani ya majengo na ardhi kwa ajili ya kumbukumbu(Data Bank)
  • Kufanya uthamini wa malipo ya fidia, kodi za nyumba, rehani, bima, mizania (Balance sheet) na mauzo ya mali
  • Kuandaa maeneo ya kusimika alama za msingi za upimaji
  • Kutayarisha michoro ya utambuzi (Description diagrams)
  • Kupokea na kuhakiki picha za anga kutoka kwa mkandarasi.
  • Kufanya upimaji, mahesabu na kuandaa taarifa za kazi (Demarcation, coordination, computation and compilation).
  • Kuchora plani za upimaji (Survey plan)
  • Kuchora plani za Hati (Deed plan)
  • Kuingiza taarifa za upimaji kwenye kompyuta (alpha numeric data)
  • Kukagua kazi za upimaji na kuingiza taarifa za kazi zilizothibitishwa kwenye compyuta.
  • Kufanya upimaji picha (aerial triangulation and block adjustment)
  • Kuandaa vikosi kwa ajili ya kuhuisha ramani (map revision)
  • Kutunza kumbukumbu za picha za anga
  • Kusimamia na kuchukua vipimo vya tide gauge (Hydrographic survey)
  • Kufanya kazi za nje ya ofisi (field survey operations) chini ya usimamizi wa mpima aliyesajiliwa.
  • Kutoa huduma kwa wateja (customer services)
  • Kukagua masuala ya upimaji katika Halmashauri za Jiji, Manispaa, Miji na Wilaya (technical auditing)
  • Kupokea na kushughulikia maombi ya upimaji picha anga.
  • Kufanya maandalizi ya upimaji wa majini.
  • Kuchambua na kuchunguza taarifa mbalimbali (data analysis)
  • Kusimamia upimaji wa kumbukumbu (data bank)
  • Kuchambua na kuchunguza matokeo ya kazi za upimaji na kutayarisha taarifa ya kiufundi.
  • Kusimamia mfumo wa utayarishaji ramani kwa kompyuta.
  • Kushauri Halmashauri kuhusu masuala ya upimaji na utayarishaji ramani.
  • Kukagua kazi za upimaji na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani
  • Kufanya ubunifu wa ramani mpya
  • Kutoa ushauri kwa wateja kwa ajili ya ramani maalum (thematic map)
  • Kufanya operasheni za upimaji
  • Kufanya uchambuzi wa takwimu (data processing and analysis)
  • Kutayarisha alama za upimaji (survey plan beacons)\
  • Kupanga na kuandaa mahitaji ya kambi za upimaji, vifaa vya upimaji na mahitaji ya jumla.
  • Kuandaa na kuchambua vifaa kwa ajili ya utayarishaji ramani.
  • Kuchambua, kushona, kukata na kuunganisha nyaraka zilizochapwa. Doria kusimamia sheria, taatibu na miongozo ya Idara.
  • Kulinda maisha ya wananchi na mali zao dhidi ya wanyamapori waharibifu na wakali.
  • Kutoa elimu ya uhifadhi, usimamizi na matumizi endelevu ya wanyama pori.
  • Ukusanyaji maduhuli na kazi za utawala.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI. June 11, 2025
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WADAU WA ZAO LA TUMBAKU WATAKIWA KUZINGATIA MIONGOZO YA KILIMO CHA ZAO LA TUMBAKU ILI KUPATA TIJA YA ZAO HILO.

    June 17, 2025
  • WANANCHI WA KIJIJI CHA PARK NYIGOTI SERENGETI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOKA GRUMETI FUND.

    June 13, 2025
  • GRUMETI FUND YAENDELEA KUGUSA MAISHA YA VIJANA WA KIKE NA KIUME WILAYANI SERENGETI.

    June 04, 2025
  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti