Kitengo cha sheria kina watumishi wawili ambao ni;
1.. Wakili Maganiko B.D.Msabi (ambae ni mkuu wa kitengo cha sheria) pamoja na
2. Wakili Veronica c. lukanda .
Kitengo hiki kina shuughuli kuu za utekelezaji wa mipango ,upitishaji na ufuatiliaji wa sheria ndogo za kodi ya majengo ,ushuru wa huduma za usafi na mazingira ,Ada na ushuru wa marekebisho ya kanuni za kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
Aidha kitengo hiki kina wajibu wa kuhakikisha dhana ya Sheria ya demokrasia inafikiwa kwa kutimiza majukumu yafuatayo:
Kutoa ushauri juu ya mambo yote ya kisheria.
Kusimamia kesi mahakamani .
Kutoa ushauri katika vikao vya menejimenti na vya halmashauri nzima vilivyopo kwa mujibu wa sheria.
Kupitia mikataba na kutafsiri vyema na kufuatilia utelekezaji wake;
Kusaidia utungaji wa sheria ndogo na kufuatilia upitishaji na utekelezaji wake .
Kujenga uwezo kwa masuala ya kisheria .
Kusimamia uundwaji wa mabaraza ya ardhi ya kata na kuyasimamia katika utendaji wa kazi zake .
Kutoa ushauri wa kisheria na msaada huo kwa wananchi.