Leo Julai 10, 2025 Mamlaka ya mji mdogo Serengeti imezindua baraza lake jipya la wajumbe tangu kukamilika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024. Mkutano huu wa uzinduzi umefanyika katika ukumbi wa Kituo cha Walimu (TRC) ambapo sambamba na uzinduzi huo kuliambatana na shughuli za uchaguzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo, uundaji wa kamati mbalimbali za kudumu na uchaguaji wa wenyeviti wa kamati hizo.
Katika Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo, Ndugu Chacha Charles Ally ameibuka mshindi wa kiti cha Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo kwa kupata kura za ndiyo kwa wajumbe wote wa Baraza hilo huku Ndg. Mikidadi Iddy Mugonya naye ameibuka mshindi wa kiti cha makamu mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo kwa kupata kula zote zilizopigwa na wajumbe wa baraza hilo.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti Bw. Milama Masiko amewapongeza viongozi waliochaguliwa na kuwataka kuwa wahakikishe wanawatumikia wananchi wa maeneo yao katika kuleta maendeleo ya wananchi hao
.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti