• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

SERENGETI YAJIPANGA VEMA KUELEKEA SIKU YA KILELE YA MTOTO WA KIKE DUNIANI

Imewekwa: October 10th, 2022

SERIKALI Wilayani Serengeti Mkoani Mara imeendelea kukemea vikali vitendo vya ukatili wa Kijinsia ikiwemo ukeketaji, ndoa za utoto pamoja na tohara zisizo Salama ambazo zimekuwa zikiwahusisha Wavulana kutahiriwa  kwa kutumia kisu  maeneo ya porini  hali ambayo imetajwa  inaweza kuwa chanzo Cha magonjwa ya kuambukiza.



Kauli hiyo imetolewa Oktoba 10,22  na Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Dkt. Vincent mashinji wakati akifungua kongamano kuelekea siku ya kimataifa ya  mtoto wa kike lililofanyika katika shule ya Sekondari Mugumu na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa serikali, mashirika ya kiraia pamoja na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Wilayani humo.



"Madhara ya Ukatili wa Kijinsia ni mengi sana, ukeketaji unaleta magonjwa ya kuambukiza, unaathiri Watoto kisaikolojia na kukatisha masomo yao. Serikali inaendelea kumthamini na kumlinda mtoto wa kike kusudi afikie ndoto zake, kwa hiyo tukikamata mtu anakeketa jela itamhusu kwani ni kosa kubwa." amesema Dkt. Mashinji.


"Na kwa wale wanaotahiri vijana maporini kwa kutumia visu waache, vijana waambieni wazazi  kama wanataka kuwafanyia tohara wawapeleke hospitalini kupata tohara salama. Mkiendelea kutahiliwa kwa kutumia visu mrapata UKIMWI na tetenasi  lazima Jambo hili liachwe ."amesema.



Aidha,  Dkt. Mashinji ameihimiza Jamii kuendelea kuwapa haki sawa Watoto wa kiume na Watoto wa kike  ikiwemo fursa ya elimu na kusimamia maendeleo yao kitaaluma kusudi wafikie ndoto zao.Huku akiagiza makongamano mbalimbali yaendelee kufanyika katika shule za Sekondari Wilayani humo yenye mada mbalimbali za kujenga na kuwaandaa vijana kuja kuwa viongozi katika taifa.





Amewahimiza wanafunzi wote Katika shule za msingi na sekondari Wilayani humo kusoma kwa bidii na kuwa na malengo, huku akiwataka wajiepushe na vitendo vya kimapenzi ambavyo vinaathari kubwa katika maendeleo yao ya kitaaluma. 




Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara  amesema kila mmoja anajukumu la kuwalinda watoto wa kike na Watoto wa kiume sambamba na kuwatimizia mahitaji yao ya msingi na kuwalea katika maadili mema.




Naye Daniel Misoji  Kutoka Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania akizungumza na Waandishi wa Habari kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo Rhobi Samwelly amesema shirika Hilo limeendelea kutoa elimu kwa Jamii juu ya madhara ya vitendo vya ukatili wa Kijinsia. Huku akitaja wasichana 65 waliokomewa na shirika hilo msimu wa ukeketaji.




Ameongeza kuwa, Shirika hilo  linaendelea kutoa hifadhi kwa wasichana waliokimbia ukeketaji na ndoa za utotoni kupitia vituo vyake kikiwemo Kituo cha Hope Mugumu na Nyumba Salama Butiama na pia linawaendeleza kitaaluma na kifani kusudi wafikie ndoto zao.


Kabla ya kufanyika kongamano hilo, ulifanyika mchezo wa mpira wa mpira wa miguu  Kati ya timu ya Hope for Girls and Women in Tanzania na timu Kutoka Shirika la World Changer, ambapo Hope for Girls and Women in Tanzania waliibuka na ushindi wa bao 1-0.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI July 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI. June 11, 2025
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DAS MASIKO AKABIDHIWA OFISI.

    July 04, 2025
  • DC ANGELINA AKABIDHIWA OFISI

    July 04, 2025
  • DC SERENGETI AAPISHWA RASMI.

    July 03, 2025
  • WADAU WA ZAO LA TUMBAKU WATAKIWA KUZINGATIA MIONGOZO YA KILIMO CHA ZAO LA TUMBAKU ILI KUPATA TIJA YA ZAO HILO.

    June 17, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti