Madiwani wa Halmashauri ya Serengeti Katika Kikao cha uwasilishaji wa Taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kila Kaa katika kipindi cha Robo ya pili.
MWENYEKITI wa halmashauri ya Serengeti Ayub Makuruma amempongeza diwani wa kata ya Kenyamonta Henry Nyamete kwa usimamizi mzuri wa makusanyo ya Mapato ya fedh kiasi cha zaidi ya milioni 24 kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka2023
Ametoa pongezi hizo kwenye kikao cha baraza la madiwani cha uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kila kata cha robo ya pili mwaka huu.
Makuruma aliwataka madiwani wa kata nyingine kuiga mfano wa diwani wa kata hiyo ili kuweza kukusanya mapato katika kata zao kwa ya kuboresha miradi ya maendeleo.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kata ya Kenyamonta diwani Nyamete alitaja mafanikio mengine waliyopata kuwa ni pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa Monchwari kwa asilimia 99 katika kituo cha afya cha Iramba, ujenzi wa madarasa 4 shule ya sekondari ya Ngoreme na ofisi ya walimu.
Amesema changamoto zilizopo ni upungufu Wa watumishi katika sekta ya elimu na afya na gari la wagonjwa katika kituo hicho cha Iramba.
Nyingine ni pamoja na migogoro ya mipaka katika kijiji cha Hekwe,Mesaga na Majimoto,ukosefu wa huduma ya maji na umeme kijiji cha Hekwe na Magatini na mbolea ya ruzuku ikiwa ni pamoja na kutokuwa na Afisa kilimo .
Ameongeza kuwa tayari wamekwisha muandikia barua Mkurugenzi wa halmashauri hiyo juu ya kutatua changamoto hizo.
Akizungumzia changamoto ya maji katika kijiji cha Hekwe alisema RUWASA wamewaahidi kwamba utekelezaji wa mradi wa maji wa kijiji hicho upo katika bajeti ya fedha ya mwaka huu.
Diwani wa kata hiyo ya Kenyamonta ameiomba serikali kufanya mgawanyo wa kata hiyo ziweze kuwa mbili ili pawe na urahisi wa kuwafikia na kutoa huduma kwa wananchi na kwamba kata hiyo ni kubwa na ina vijiji vitano na jiografia yake imekaa vibaya.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti