• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Maafisa Habari na TEHAMA ni Wakala wa Mabadiliko.

Imewekwa: February 13th, 2018

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Joseph Nyanda, amewakumbusha Maafisa Habari na Maafisa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, maarifa na ubunifu, kwakuwa wao ni mawakala wa mabadiliko.

Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), yamefunguliwa jana  Februari 12 2018 na Ndugu Nyanda huku akiwatahadharisha maafisa hao kutozembea kutekeleza wajibu wao wa msingi kwa weledi.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Ndugu. Raphaele Jospeh Nyanda akisisita jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa maafisa habari na TEHAMA.

“Kila mmoja miongoni mwenu anayo dhamana ya kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na Serikali, lakini mkikaa kimya ninyi kama sauti za taasisi zenu, watu wasio wema watapotosha maudhui hayo na mwisho wa siku kuchafua taswira ya Serikali” amesisitiza Nyanda.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi Rebbeca Kwandu, amewasisitizia maafisa hao kubadilika katika utendaji wao mara baada ya mafunzo ya mfumo huo juu ya uendeshaji wa tovuti.

“Mwanzoni tulipoanzisha tovuti hizi, hatukuwa na mwongozo ambao ni dira ya uendeshaji. Hata hivyo mara baada ya OR-TAMISEMI kuandaa mwongozo huu kwa kushirikiana na wadau wetu PS3, ni imani yangu tutabadilika,” alisema Bi. Kwandu, na kuongeza kwamba uwepo wa tovuti bila ya uwepo wa habari haina maana.

Akizungumza kwa niaba ya Mradi wa PS3, Mkuu wa Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi, Dkt. Peter Kilima, amekiri kwamba Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA ndio roho ya taasisi, hivyo ushirikishwaji hasa kwenye vikao vya maamuzi itakuwa ni fursa kwao kuchuja na kuujuza umma mambo mazuri ya nchi.

Awali akitoa Salaam za Idara ya Habari (Maelezo), Mkurugenzi Msaidizi wa Habari na Picha, Rodney Thadeus, aliesema kwamba ili kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na Serikali, ni lazima Maafisa Habari wawe na zana za utendaji kazi, na zana zenyewe katika mustakabali wa sasa kwa ngazi za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ni tovuti.

“Wafadhali PS3 wametuwezesha kuwa na mfumo wa Government Website Framework (GWF). Tumieni hizi tovuti kama tools (zana) za kuujuza umma.

Mafunzo haya ya siku nne ni ya awamu ya kwanza kwa Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA kutoka mikoa ya Mara na Arusha, na mafunzo kama haya yatafanywa pia kwa maafisa kutoka mikoa mingine yote iliyobaki ya Tanzania bara.

Mafunzo ya mwongozo wa tovuti za Serikali yameandaliwa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa PS3 ambao unafadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani (USAID). Takribani Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA 418 kutoka Ofisi za Mikoa na Halmashauri Tanzania bara wanatarajiwa kupatiwa mafunzo hayo.


Matukio katika picha.

Maafisa habari na TEHAMA kutoka Sekretarieti na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka Mikoa ya Arusha na Mara.

Dkt. Peter Kilima, Mkurugenzi wa Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi kutoka PS3, akizungumza wakati wa Mafunzo hayo.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Bi. Rebecca Kwandu (aliyesimama kushoto) akizunguza na washitiri.


Imeandaliwa na Atley Kuni kwa kushirikiana na Englibert Kayombo

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA January 02, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO WATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    April 16, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SERENGETI LAPITISHA BILIONI 48.8 KAMA MPANGO WA BAJETI YA HALMASHAURI 2025/2026.

    March 04, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI WILAYANI SERENGETI LAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA TARURA BILIONI 2.4

    March 03, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti