“Sikatazi mtu kuuza chake lakini naomba tuhakikishe tuna chakula cha ziada ndio tuuze kwa ajili ya kujipatia mahitaji mengie ya Shughuli zetu”
Hayo yamebaiisha leo tarehe 26/02/2020 na Mkuu wa Wilaya Serengeti Mh. Nurdini Babu wakati akiwasilisha salamu za Serikali katika mkutao wa robo ya pili wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Serengeti uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
Mh. Babu amewaomba Waheshimiwa madiwani kumsaidia katika vikao vyao kuhakikisha wanawajulisha wananchi walio kweye Kata zao kuhakikisha kuwa wanabaki na chakula cha ziada kabla ya kuuza na amesisitiza kuwa akatazi mtu asiuze mazao yake ya chakula.
Akiendelea kuwasilisha salamu mbalimbali za serikali Mh. Babu amesema kuwa katika maboresho ya Jeshi ya Polisi imeagizwa kuwa kila Kata kuwa na kituo kidogo cha polisi ili kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yote nchini ikiwemo matukio ya utoro na mimba za wanafuzi na matukio mengine kama hayo ambayo yanaweza kukamilika katika gazi za chini.
Pia Mh. Babu amesema kuwa wiki ijayo ataanza ziara ya kutembelea shule zote za Sekondari Serikali ili kubaini hali halisi ya uripoti wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2020 na atasita kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kushiriki katika zoezi la kutowapeleka watoto shule.
“Sasa tumejenga Sekondari, watoto wamefaulu wazazi hawapeleki watoto shule na Waheshimiwa madiwani tupo kwenye hizo Kata tunajua watoto hawajakwenda shule. Tulisema Januari watoto wote waende shule lakini mpaka leo watoto wengine hawajakwenda shule” Alisema Mh. Babu
Aidha Mh. Babu amewataka watu na wadau wa maendeleo wanakaribishwa kuja kuwekeza katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya maelezo kutoka katika Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambao alikuwa na kikao nao asubuhi ya leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa baraza ya madiwani. Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ilipata fursa ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti ambapo TANAPA imechangia kiasi cha Milioni 80. Mchango huu ni mojawapo ya miradi mbalimbali inayotolewa na shirika katika kuwawezesha jamii zinazoishi jirani na hifadhi kutambua umuhimu wa hifadhi husika.
Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa na Mh. Babu na Viongozi wengine katika picha ya pamoja.
Na mwisho Mh. Babu amesisitiza upendo na ushirikiano kwa watumishi uzidi kuimarishwa zaidi ili kuleta maendeleo ya wilaya yetu kwa ujumla na amewasihii wote wenye tabia za kubezabeza waachane na tabia hizo mara moja.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti