Kitengo cha manunuzi na ugavi kimefanya ufunguzi wa zabuni za ujenzi wa barabara ya lami nyepesi yenye urefu wa Kilometa 2 katika mji wa mugumu na zabuni za matengezo ya mtandao wa barabara katika Wilaya ya Serengeti.
Akifungua kikao hicho Afisa manunuzi mwandamizi Bw. Benedicto Lubengo alisema “kikao hiki ni cha kisheria na sitegemei kupokea maswali kwa siku ya leo kwa kuwa tulishatoa muda wa siku 21 za kuuliza maswali”
Katika kuweka uwazi wa zabuni hizo, wazabuni waliorudisha vitabu vya zabuni za ujenzi na matengenezo ya barabara walialikwa kuhudhuria kikao hicho na kusomewa zabuni zilizofika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
BI Caroline Daffa ambae ni Afisa Manunuzi alitaja vigezo vya kuzingatiwa ili mzabuni aweze kupata zabuni, ambapo alibainisha mzabuni anapaswa kuwa na; Cheti cha mlipa kodi (VAT), Cheti cha utambulisho wa mlipa kodi (TIN), Leseni ya biashara, Hati ya nguvu ya kisheria kukasimu madaraka (Special Power of Attorney), Cheti cha usajili wa wakandarasi (CRB), Amana ya zabuni (Tender Security) pamoja na cheti cha usajili wa kampuni.
Aidha Kaimu Afisa manunuzi Wilaya ya Serengeti, Bw. Nimrod Ndossi alisema kuwa baada ya ufunguzi wa zabuni hizo hatua itakayofuata ni kazi ya tathimini ambapo zabuni zote zitapitiwa upya na timu ya tathimini na kuchujwa kabla ya kupelekwa kwenye bodi ya zabuni kupitiwa na kutunuku.
Ikumbukwe kuwa Mji wa Mugumu una lami nyepesi yenye urefu wa kilometa 3 iliyopo katikati ya Mji, kuongezewa kwa lami yenye urefu wa kilometa 2 kutaufanya Mji huo kupendeza zaidi na kupunguza adha ya ubovu wa barabara.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti