Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kupitia Idara ya Afya inatarajia kuendesha zoezi la utoaji wa chanjo ya HPV kwa wasichana zaidi ya elfu 30, chanjo ambayo itasaidia kumkinga msichana kupata ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati ya Afya ya Wilaya Leo Aprili 22, 2024, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt. Vincent Mashinji amewataka wajumbe wa kamati hiyo kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha chanjo hiyo ili lengo la kuwachanja wasichana zaidi ya elfu 30 liweze kutimia huku akiwataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo muhimu.
kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt. Adam Lusubilo amesema walengwa wa chanjo hii ni wasicha wenye umri wa kuanzia miaka 8 hadi 14 huku akifafanua kuwa lengo la chanjo hiyo ni kumkinga mtoto wa kike na maambukizi ya Saratani ya kizazi.
Katika siku tatu za utoaji wa chanjo hiyo inakadiliwa kuwa wasichana zaidi ya elfu 30 watapata huduma hiyo ambayo itatolewa katika shule za msingi na Sekondari pamoja na vituo vyote vya Afya ndani ya Wilaya ya Serengeti.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti