Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti leo Februari 17, 2026 limepokea na kupitisha rasmi mabadiliko ya jina la Mji wa Mugumu ambao sasa utajulikana kama Mamlaka ya Mji Mdogo wa Serengeti.
Taarifa hiyo iliyowasilishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani na kusomwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Ayub Mwita Makuruma, imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni kwa mujibu wa tangazo la Serikali namba 796 linalohusu Amri ya Mgawanyo wa maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa.
Akiwasilisha taarifa hiyo Mhe. Makuruma amebainisha kuwa mabadiliko hayo ni sehemu ya mpango wa maboresho ya kimaendeleo yatakayoufanya mji huo kuwa kitovu cha utalii na uwekezaji kufuatia umaarufu na ukubwa wa jina hilo duniani kote hivyo, hii itafanya mji huo utambulike kimataifa na kuvutia wawekezaji, kukuza mapato ya halmashauri, na kutoa fursa zaidi za kiuchumi kwa wananchi.
Aidha, Waheshimiwa Madiwani kwa kauli moja wamepongeza hatua hiyo, wakisisitiza kuwa uamuzi huo utafungua milango ya maendeleo na kuimarisha hadhi ya mji huo kama lango kuu la Utalii nchini.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti