Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Ndg. Jabir Athuman Ali, leo tarehe 20 Februari 2026, ameongoza kikao cha Kamati ya Lishe kwa robo ya pili ya mwaka kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe wa kamati ya lishe ngazi ya Wilaya pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya lishe, wajumbe wamejadili mikakati ya kuboresha hali ya lishe katika halmashauri, sambamba na kuimarisha utoaji wa elimu ya lishe kwa wananchi.
Aidha kamati hiyo imesisitiza utoaji wa elimu ya lishe kwa watoto na vijana kupitia shule, ili kuongeza uelewa wa lishe bora na kuchangia katika kuboresha afya na maendeleo ya jamii kwa ujumla.

31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti