Tarehe 25 Aprili ya kila mwaka ni siku ya Malaria duniani, wakati ambapo Shirika la Afya duniani (WHO) hutoa uelewa kwa jumla kuhusu juhudi za pamoja na kuiepusha dunia na malaria.
Nchini Tanzania, Wilayani Serengeti, Mkoani Mara, Halmashauri ya Wilaya hiyo, imetumia siku hii kuendesha zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi na Wanafunzi waliojitokeza katika shule ya Msingi Kambarage B sambamba na kutoa elimu juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa malaria pamoja na namna ya kutambua dalili za ugonjwa huo.
Katika siku hiyo iliyobeba kauli mbiu isemayo "Huduma za afya kwa kuzingatia uhitaji, jinsia na haki kwa wote. Ziro malaria inaanza na Mimi" wananchi wameaswa kuzingatia matumizi ya dawa za Maleria pamoja na kuzingatia matumizi ya chandarua.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti