Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Leo Aprili 16, imezindua programu jumuishi ya kitaifa juu ya malezi, makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto, programu ambayo imejikita katika kukuza afya bora kwa mtoto na mlezi, lishe bora na malezi yenye mwitikio.
Aidha, programu hiyo inalenga kuhakikisha kuwa watoto wanapata fursa bora za makuzi na malezi, sambamba na ulinzi dhidi ya hatari zozote zinazoweza kuwakabili.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti, Mkuu wa Idara ya Utumishi Ndg. Ally Ligalawike amesema kuwa uzinduzi huu ni hatua muhimu katika kuhakikisha ustawi na maendeleo bora kwa watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti huku akiwataka wazazi na walezi kuwapa watoto mafunzo ya kidini.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti