Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt. Vincent Mashinji ameipongeza Taasisi ya World Changer Vision kwa namna inavyoigusa jamii ya Serengeti na Watanzania kwa ujumla hasa katika sekta ya elimu na afya.
Akizungumza katika mahafali ya Chuo cha Ufundi stadi cha World Changer Vision ambayo yameambatana na kutambulisha kituo cha huduma ya kwanza, Dkt. Mashinji amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia wananchi kwa wakati na kwa ubora hivyo taasisi ya World Changer inarahisha katika kutimiza malengo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya World Changer Ndg. Sulus Samwel amesema lengo la taasisi hiyo kuanzisha kituo cha huduma ya kwanza ni kuhakikisha jamii ya Serengeti inakuwa na afya njema ili iweze kujikita katika shughuli za kuinua uchumi sambamba na kuwasaidia watoto wanaolelewa na taasisi hiyo kupata matibabu kwa urahisi.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti