Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Ayub Makuruma ambaye pia ni Diwani wa kata ya Busawe,imefanya Ziara ya kutembelea na kukagua Ukamilishaji wa Zahanati ya Kegonga iliyopo kitongoji cha Manyunyi kata ya Matare .Wananchi walijenga mpaka kufikia hatua ya boma,Aprili 2022 Kituo hiki kilipokea kiasi cha Tzs.50,000,000/= Kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Ayub Makuruma amezipongeza kamati ambazo zilikuwa zinasimamia ujenzi wa zahanati hiyo,sambamba na kupongeza uongozi wa Kata kwa kuweza kuhamasisha wananchi kujitoa na kuweza kujenga zahanati hiyo .
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti