AFISA TARAFA ROGORO BW. GASPER IRIGO AMEFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MRADI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI KEMANGÓRE KIJIJI CHA MASANGURA KATA YA NYAMOKO.
Ujenzi wa Shule Hiyo ulianza Rasmi Mwezi wa saba Kufikia Sasa Wamekamilisha Majengo Mawili yenye Vyumba 4 vya Madarasa na Ofisi 1 ya waalimu kwa Nguvu Zao Wenyewe, Pamoja na Juhudi hizo Wananchi Wamelalamikia Uongozi wa Serikali ya Kijiji kuwa ni Miongoni mwa Wanaokwamisha Mradi huo kwa Kushikilia Fedha Zilizotolewa na Wananchi Kwa Ajili Ya Miradi ya Maendeleo ya Kijiji na Wameshindwa Kuzitoa kwa Wakati. Pia Wananchi wamelalamikia Kutokuwepo na Usimamizi mzuri wa Vifaa vya Mradi wa Ujenzi Huo (Saruji) na Mwitikio Mdogo wa Wananchi Katika Kushiriki Ujenzi wa Mradi Huo.
Aidha Baada ya Malalamiko hayo Afisa Tarafa Bw. Gasper Ametoa Maagizo Kwa Viongozi wa Kata na Kijiji Kuwa ndani ya Siku nne Kuanzia Leo Tarehe 17/09/2021 wawe Wamebaini na Kuwatambua Watuhumiwa Wote wanaodaiwa Fedha na Rasilimali za Mradi Huo. Pia amewatia Moyo Wananchi kwa Kuwaihidi Kuwa Serikali Itaunga Mkono Ujenzi wa Mradi Huo Baada ya Mradi Kufikia Hatua Ya Kupaua Majengo.
Baada ya Kusema Hayo Nae Afisa Mtendaji Kata ya Nyamoko Bw. Amos Kemberete Ametoa Maagizo Kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji Kuwaandikia Barua ya Wito Wadaiwa wote na Kuwataka Wafike Katika Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Tarehe 22 septemba, 2021 saa 4 Asubuhi.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti