YANGA TAWI LA SERENGETI WAZIKUMBUKA HOSPITALI
Kila ifikapo agosti 6 kila mwaka ni ya siku maalumu ya wananchi (YANGA) ambapo katika wilaya ya Serengeti,Tawi la Yanga limeadhimisha siku hii kwa kuzitembelea hospitali wilayani hapa.
Pamoja na kuadhimisha kilele cha siku ya Mwananchi,Tawi hili limesheherekea pia ubingwa ambao YANGA uliutwaa katika msimu wa 2021/2022.Maadhimisho haya yaliongozwa na Kauli mbiu zinazosema ‘’Ujanja ni kujisajili kuwa wanachama’’ pamoja na ‘’sensa kwa maendeleo ,jiandae kuhesabiwa;’’
Katika Picha ni Baadhi ya wanachama wa Yanga Tawi Serengeti wakifanya Usafi katika Maeneo ya Hospitali ya Kibeyo.
Wakiwa katika hospitali ya wilaya ya Serengeti ya kibeyo, wanachama wa YANGA Tawi la Serengeti wamefanya usafi wa mazingira pamoja na kutoa msaada wa Mashuka kwa ajili ya wagonjwa.
Aidha,Katika hospitali Teule ya wilaya ya serengeti Nyerere wanachama wamefanya zoezi la uchangiaji damu,ambapo takribani wanachama 30 walichangia.
Kiongozi wa Yanga Tawi la Serengeti akikabidhi Msaada wa Mashuka kwa niaba ya wanachama kwa Muuguzi Hospitalini hapo
Akihitimisha siku hiyo ya Mwananchi Mgeni Rasmi wa Maadhimisho Hayo S.I Emmily Mwakyusa amewashukuru wanachama waliojitokeza katika maadhimisho hayo ya siku mwananchi, pamoja na kuwaomba kuendeleza ushirikiano na umoja Baina yao,lakini pia amewakumbusha wanachama hao kujitokeza na kutoa ushirikiano katika sensa ya watu na Makazi itayofanyika Agosti 23,2022.
Katika picha:Baadhi ya wanachama wa Yanga Tawi la Serengeti wakiwa tayari kuchangia damu katika hospitali ya Nyerere DD
Nao Viongozi wa Yanga Tawi la Serengeti wamewakumbusha wanachama wao kukumbuka kujisajili ili kuwa wanachama halali, lakini pia kuendeleaa kujitoa katika shughuli mbalimbali za kijamii ili kuweza kuleta maendeleo katika Jamii .
Imetolewa na
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Wilaya ya Serengeti
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti