Chuo cha World Changer kilichopo Wilayani Serengeti mkoani Mara kilianzisha mwaka 2019 kikiwa na mwanafunzi mmoja ambapo mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 68 wakiwa wamehitumu mafunzo ya ufundi stadi katika chuo hicho huku wanafunzi zaidi ya 80 wakiwa wanaendelea kupata elimu katika chuo hicho.
Hivyo, kutokana na umuhimu wa chuo hicho katika kuokoa ndoto za vijana serikali Wilayani Serengeti imeaidi kushirikiana bega kwa bega na uongozi wa chuo hicho katika kuweka mazingira bora ya ufanyaji kazi ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu inayoelekea chuoni hapo jambo litakalosaidia katika kutimiza ndoto za vijana wanaotegemea chuo hicho kutimiza ndoto zao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt. Vincent Mashinji amesema uwepo wa chuo hicho katika Wilaya ya Serengeti ni chachu muhimu katika kutimiza ndoto za vijana na kuzalisha ajira na kuleta maendeleo kwa vijana nchini kote hivyo kama serikali itashirikiana vyema na chuo hicho ili ndoto za vijana hao ziweze kutimia.
Dkt. Mashinji ameongeza kuwa uwepo wa chuo hicho ni daraja la kuunganisha na kuimarisha uhusiano mwema uliopo baina ya serikali ya Tanzania na Ujerumani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya World changer Vision nchini Ndg. Sulus Samwel amesema chuo cha World changer vision kimejikita katika kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu kuhakikisha wanapata elimu ili waweze kutimiza ndoto zao.
Nao wanafunzi waliohitimu katika chuo hicho wamesema uwepo wa chuo hicho umekuwa wenye manufaa kwao kwani wamejifunza stadi mbalimbali za maisha pamoja na ujasiriamali hivyo kwa Sasa wanaouwezo wa kujitengenezea kipato kuliko hapo awali.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti