Shule ya Msingi Robanda Kata ya ikoma wilayani Serengeti kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na Kata ni miongoni mwa shule zinazotekeleza utaratibu wa kuwapatia wanafunzi chakula Shuleni.ikiwa ni Mkakati wa kitaifa wa kuhakikisha mtoto awapo shuleni anapata chakula .
Katika shule ya Msingi Robanda wazazi wamekuwa mstari wa mbele kuchangia chakula Shuleni na hivyo kufanya watoto wote kuanzia darasa la Awali hadi la Saba kupata chakula.
‘’Kila Muhula tunakuwa na kikao cha wazazi kwa ajili ya kuandaa bajeti ya uji wa wanafunzi wakiwa shuleni ‘’Alisema mkuu Msaidizi wa Shule hiyo Mwl.Noel Abel
Kwa Upande wa Wanafunzi wameishukuru serikali kwa kusimamia swala la Lishe mashuleni pamoja na wadau wa utalii Focus on Tanzania communities kupitia Thomson safaris LTD Kwa kuwajengea Jiko la kisasa kwa ajili ya kupikia chakula wakiwa Shuleni.
Diwani wa kata ya Ikoma Mhe.Michael Kunani amewataka wazazi kuendelea kuchangia chakula shuleni kwani ni chakula ambacho mtoto angeweza kula nyumbani kiletwe shule aweze kula na kumpa mtoto utulivu wa kimsomo na kuweza kufanya vyema katika masomo yake.
Aidha,Afisa Lishe Wilayana Bi.Flomena Cyprian ameipongeza shule hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika huzingatia swala la lishe na kuzitaka nyingine wazazi kuhamasika kuchangia chakula Shuleni ili kuwajegea watoto afya Njema na Kuongeza utulivu wa kimasomo na kuomgeza ufaulu wao na shule kupata matokeo mazuri
Halmashauri ya wilaya ya Serengeti inaendelea kutenga na Mapato yake ya ndani katika kutekeleza afua mbalimbali za Lishe kama ambavyo Mhe.Rais alitoa maelekezo wakatika kusaini mikataba ya Lishe Hivi karibuni.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti