Serikali kupitia mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management Information System – HCMIS/Lawson) imehakiki madeni ya watumishi 82,111 wanaodai madeni yenye jumla ya shilingi 127,605,128,872.81
Uhakiki umebaini madai ya jumla ya watumishi 27,389 kati ya 82,111 yenye thamani ya shilingi 43,393,976,807.23 sawa na 34% ya madai yote yaliyohakikiwa kuwa ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.
Kati ya watumishi 27,389 waliohakikiwa, watumishi 133 ni wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambao madai yao yameonekana kuwa na vielelezo.
Orodha ya majina ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imeambatanishwa.
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA MAJINA YA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI.
Awali jana akiongea na waandishi wa habari Mjini Dodoma Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema madai hayo yanajumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishwa mishahara.
“Kufikia tarehe 01 Julai, 2017 Serikali ilikuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara yenye jumla ya shilingi Bilioni 127.6 kwa watumishi 82,111 wakiwamo walimu 53,925 waliokuwa wakidai Shilingi Bilioni 53.94 sawa na asilimia 42.27 ya madai yote na wasiokuwa walimu 28186 wanaliokuwa wakidai Bilioni 73.6 sawa na asilimia 57.73” Alisisitiza Dkt. Mpango.
Akizungumzia matokeo ya uhakiki wa madeni hayo Dkt. Mpango amesema kuwa madai ya watumishi 27,389 kati ya 82,111 yenye jumla ya shilingi bilioni 43.39 ikiwa ni asilimia 34 ya madai yote ya shilingi bilioni 127.6 yaliyohakikiwa yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.
Waziri Dkt. Mpango aliongeza kuwa madai yanayostahili kulipwa yanajumuisha shilingi bilioni 16.25 kwa walimu 15,919 na shilingi bilioni 27.15 kwa watumishi wasiokuwa walimu 11,470.
akifafanua kuhusu matokeo ya madai hayo yamewezesha Serikali kuokoa jumla ya shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na asilimia 66 ya madai yote ya malimbikizo ya awali ya shilingi bilioni 127.61 yaliyokuwa kwenye mfumo.
Aidha, Waziri Dkt. Mpango amesema kuwa hatua hiyo ni matokeo ya juhudi za Serikali ambazo ni pamoja na kuwaondoa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara watumishi hewa, vyeti feki na wasio na sifa.
Serikali itaendelea kulipa madai ya watumishi kadiri yanavyojitokeza ili kuondokana na malimbikizo ya aina hii ambayo yanaweza kuisababishia Serikali hasara kwa kulipa madai yasiyostahili.
chanzo http://bongo5.com/watumishi-wa-umma-27389-kulipwa-madeni-yao-mwezi-huu-02-2018/
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti