KWA mara ya kwanza, Maafisa Watendaji wa Kata wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kata zao kwa niaba ya madiwani, katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara.
Kisha madiwani walijadili na kutoa mapendekezo ya kutatua changamoto mbalimbali na kushauri namna bora ya usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata zao, huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, Afraha Hassan akiahidi kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi na kufanyia kazi ushauri na maelekezo yaliyotolewa na baraza hilo la madiwani.
Kikao cha Baraza la Madiwani hao kinaendelea kwa siku ya pili leo Alhamisi, ambapo kitakuwa cha wazi na kamati mbalimbali zitawasilisha taarifa za shughuli zilizotekelezwa na halmashauri kwa kipindi cha Julai - Septemba 2023.
Madiwani kwa kauli moja waliridhia taarifa hizo ziwasilishwe na Maafisa Watendaji wa Kata katika kikao cha robo ya kwanza [Julai - Septemba 2023], kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Ayub Mwita Makuruma, mjini Mugumu jana Jumatano.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti