Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Serengeti Mhandisi Juma Hamsini amewataka Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria zinazosimamia uchaguzi nchini katika kusimamia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 28 Mwaka huu.
Mhandisi Juma ameyasema hayo Jana Tarehe 07/08/2020 wakati akifungua mafunzo ya usimamizi wa Uchaguzi kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka Kata 30 za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti zinazotarajia kushiriki katika Uchaguzi huo, yanayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambapo kesho Tarehe 09/08/2020 yatahitimishwa
Alisema pamoja na baadhi ya Wasimamizi kuwa na uzoefu katika kusimamia chaguzi mbalimbali, aliwasisitiza kuzingatia maelekezo watakayopewa na katika mafunzo haya katika kusimamia uchaguzi huo badala ya kusimamia kwa mazoea kwani Tume imewaamini kuwa wanaweza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria.
“Ndugu washiriki mnatakiwa kutambua kuwa mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu mnao uwezo wa kufanya kazi hii jambo la muhimu ni kujiamini na kujitambua na kwamba mtapaswa kuzingatia sheria, miongozo, kanuni na maelekezo yanayotolewa na Tume kwa ajili ya kuendesha na kusimamia chaguzi” alisema Mhandisi Juma.
Aidha Mhandisi Juma aliwataka wasimamizi hao wa uchaguzi kuwepo muda wote wakati wa kutekeleza majukumu ya uchaguzi na hata pale inapotokea dharura wahakikishe anakuwepo msimamizi atakayetekeza majukumu yao.
Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ili kutekeleza vyema majukumu yao katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi kuanzia sasa hadi viongozi wapya watakapopatikana.MAfunzo yaliyofanyika kwa nadharia na vitendo.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti