Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) kupitia Idara ya Ujenzi na Zimamoto imewataka wananchi wote kufuata taratibu za kiuhandisi katika ujenzi wowote ikiwemo kuhakikisha wanakuwa na vibali vya ujenzi (Building permit) kama sheria ya mipango miji Cap no (101) inavyosema.
Hayo yamesemwa leo Tarehe 10/08/2019 na Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi na Zimamoto Mhandisi Dickson Kamazima wakati wa zoezi la ukaguzi wa vibali vya ujenzi linaloendelea huku akibainisha kuwa watapita kitongoji kwa kitongoji na mpaka sasa takribani makazi mapya tisini na mbili (92) yamebainika kujengwa bila vibali licha ya matangazo kupita kuhamasisha wananchi kuwa na vibali vya ujenzi na wahusika hao wamepewa barua na kuitwa ofisi za Halmashauri siku ya jumanne kupewa utaratibu wa kupata vibali
Aidha Mhandisi kamazima amebainisha kuwa kuwa na kibali cha ujenzi uepusha migogoro ya ardhi isiyo na lazima na amewataka wote wanaotaka kuanza kufanya ujenzi wowote wafike Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) waweze kupatiwa utaratibu wa kupata vibali vya ujenzi aidha amewataka walioanza kujenga bila vibali kusitisha ujenzi na kuhakikisha kupata vibali vya ujenzi kwanza.
mojawapo ya nyumba zilizojengwa bila kuwa na vibali vya ujenzi
Akionesha mojawapo ya nyumba zilizojengwa bila kuwa na vibali zilizopo katika Kitongoji cha Sedeco, Kata ya Mugumu amesema nyumba kama hizo zinaweza kuteketea zote kwa moto iwapo nyumba mojawapo itawaka kwani zimejenga bila kufuata utaratibu. Hivyo Mhandisi kamazima alisistiza Wananchi wote kuhakikisha wanafuata taratibu zote katika ujezi wao.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti