• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

WANANCHI WA KIJIJI CHA PARK NYIGOTI SERENGETI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOKA GRUMETI FUND.

Imewekwa: June 13th, 2025

                                                        

SHIRIKA la Grumeti Fund katika kuendelea kugusa maisha ya Wananchi hasa waishio pembezoni mwa Hifadhi ya taifa ya Serengeti, imeendesha mafunzo ya ujasiriamali ya utengenezaji wa batiki kwa wanakijiji cha Park Nyigoti mafunzo ambayo yanalenga kuondoa utegemezi wa shughuli za uwindaji na ukataji wa mkaa katika Hifadhi hiyo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Mradi wa Ustawishaji wa Biashara kutoka Grumeti Fund Ndg. Nelson Petro akifafanua dhamira kuu ya mafunzo hayo amesema ni kutoa fursa mbadala za kiuchumi kwa wananchi itakayosaidia kuondoa utegemezi wa hifadhi badala yake kufanya shughuli nyingine zo za kuwaingizia kipato.

                                                   

"Tunatambua umuhimu wa jamii zinazoishi jirani na hifadhi kushiriki kikamilifu katika uhifadhi. Njia bora na kufanya hivyo ni kuhakikisha wanakuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato vinavyowapunguzia utegemezi wa moja kwa moja wa rasilimali za hifadhi kama vile kuni, uwindaji haramu, au kilimo kisicho endelevu ndio sababu kubwa ya Grumeti kuendesha mafunzo haya" alisema Nelson

Mafunzo haya yameundwa kwa kuzingatia mbinu za kisasa za utengenezaji wa batiki, kuanzia hatua za awali za uandaaji wa malighafi, uchoraji, uchapaji, hadi hatua za kumalizia bidhaa. Washiriki wanajifunza jinsi ya kutumia rangi zisizodhuru mazingira na mbinu za ubunifu zitakazowafanya batiki zao kuwa na mvuto sokoni.

                                                    

Naye Bi. Chausiku Elias ambaye ni mshiki wa mafunzo haya ameeleza jinsi mafunzo haya yatakavyobadilisha maisha yake ambapo wamesema 

"Nimekuwa nikitegemea sana kuchoma mkaa ambao unaharibu sana mazingira, Sasa nimepata ujuzi mpya ambao nitaweza kuutumia kujipatia kipato muda wote. Ninaamini batiki zitafungua milango ya fursa kwangu na kwa wanawake wenzangu kijijini." Alisema 

                                                   

Kwa upande wa wanaume, Bw. Jumapili Sontome amesema, "Tunashukuru sana Grumeti Fund kwa kutupa ujuzi huu. Sisi kama kama wanaume mara nyingi siku hizi tunaachwa nyuma, ujuzi wa batiki unatupa uwezo wa kujiajiri na hata kuajiri wengine. Hii itapunguza changamoto za kiuchumi tunazokabiliana nazo."

Grumeti Fund imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na serikali za mitaa na wadau wengine wa maendeleo ili kuhakikisha programu zake zinafanikiwa na kuwa na athari chanya ya kudumu. Mafunzo haya ya batiki ni sehemu ya mkakati mpana wa shirika la Grumeti Fund kuwekeza katika elimu, afya, na uwezeshaji wa kiuchumi kwa jamii zinazopakana na hifadhi, huku likisisitiza umuhimu wa uhifadhi wa wanyamapori na mazingira.

Kukamilika kwa mafunzo haya kutaambatana na msaada wa kwanza wa masoko ili kuhakikisha washiriki wanaweza kuanza shughuli zao mara moja na kujipatia kipato. Hatua hii inaashiria hatua muhimu kuelekea kujenga jamii imara kiuchumi na rafiki wa mazingira.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI. June 11, 2025
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WADAU WA ZAO LA TUMBAKU WATAKIWA KUZINGATIA MIONGOZO YA KILIMO CHA ZAO LA TUMBAKU ILI KUPATA TIJA YA ZAO HILO.

    June 17, 2025
  • WANANCHI WA KIJIJI CHA PARK NYIGOTI SERENGETI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOKA GRUMETI FUND.

    June 13, 2025
  • GRUMETI FUND YAENDELEA KUGUSA MAISHA YA VIJANA WA KIKE NA KIUME WILAYANI SERENGETI.

    June 04, 2025
  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti