Wananchi wa kata ya Kyambahi kijiji cha Nayanungu katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita wameungana kwa pamoja na kuanza ujenzi wa shule ya sekondari yenye vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja.wametoa wito kwa serikali na wadau kuwashika mkono ili kukamilisha ujenzi huo sambamba na kuongeza miundombinu mingine ikiwemo vyoo,nyumba za walimu.
Akifanya ziara ya kutembelea madarasa hayo Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt.Vincent Mashinji amewapongeza wananchi hao kwa kuona umuhimu wa elimu,na kuwahidi kushika mkono katika upauaji na kuwapatia mifuko 20 ya simenti ili waweze kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati.
Kwa upande wa diwani wa kata hiyo Herman kinyariri amesema iliwalizimu wafikie hatua ya kujenga madarasa hayo kutokana na umbali uliopo wa kuifikia shule ya sekondari nyichoka lakini wakati wa mvua Mto ukijaa inawawi wananfunzi kwenda shule lakini pia tishio la tembo hivyo kuwalazimu kuanza ujenzi wa madarasa hayo haraka.Wananategemea ujenzi wa madarasa hayo kukamilika ifikapo januari 2024.
Wananchi wamemshukuru Mkuu wa wilaya ya Serengeti kwa naman alivyojitoa kwa ajili ya shue ya hiyo ikiwa ni pamoja na kukubali kuwa mlezi wa shule ya hiyo.
Hivi karibuni Serikali imetoa Kiasi cha Mil.40 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti