Wananchi na wakulima wa tumbaku wabanwa kupanda miti
Imewekwa: April 5th, 2017
Wakazi wa Wilaya ya Serengeti wametakiwa kupanda miti isiyopungua 30 kwa kila kaya huku kila mkulima wa tumbaku kupanda miti isiyopungua 300 kwa mwaka.
Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti ndugu Nurdin Babu katika kilele cha siku ya upandaji miti wilayani serengeti katika eneo la hifadhi ya msitu wa Halmashauri uliyo katika Kijiji cha Nyamelama, Kata ya Rung'abure.
Katika kuhakikisha agizo hilo linasimamiwa, Babu amewaagiza watendaji ngazi Tarafa,Kata na Vijiji kusimamia agizo hilo kwa hukakikisha kila kaya na Mkulima wa tumbaki Wilayani Serengeti wanatekeleza agizo hilo.