Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt.Vincent Mashinji amewaomba wafugaji wote wilayani Serengeti kujitokeza katika vituo Maalumu vilivyotengwa kwaajili kuvalisha mifugo yao hereni za utambuzi za kielekroniki ikiwa njia ya kutambua mifugo ilipo na umiliki wake,kukabili magonjwa ya mlipuko ,kuwa na hakikisho la usalama wa chakula,kurahisisha biashara ya mifugo na mazao yake ndani ndani na nje ya Nchi,udhibiti wa wizi wa mifugo,kurahisisha upatikanaji wa mifugo iliyopotea,kurahisisha uboreshaji wa koosafu za mifugo lakini pia utambuzi huu utasaidia upatikaniji wa mikopo na bima za mifugo,ikiwa gharama za kwa Kila Ng’ombe/punda ni Tzs.1,750/=Tu na Mbuzi/kondoo Tzs.1000/=Tu
Akizungumza na baadhi ya wafugaji katika kijiji cha Burunga kata ya uwanja wa ndege Dkt.Mashinji amewaomba wafugaji waone umuhimu mkubwa ulipo katika kuvalisha mifugo yao Hereni hizo na Dhumuni la serikali ni kuitaji kutambua mifugo iliyopo na kuweza kusaidia kuthibiti wizi wa mifugo.
Kwa upande wa Diwani wa kata ya Uwanja wa ndege Mhe.Matoke Joseph amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Serengeti kusaidia elimu juu hereni za kielekroniki kuwafikia wafugaji ili uweza kuleta uwelewa wa faida na umuhimu wa kuwawekea mifugo yao hereni hizo.
Aidha,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Ndg.Simeon Waryuba amewataka wafugaji kufanya ufugaji wenye tija ’’faida za uwekaji wa hereni hizi naweza kuziweka kwenye makundi mawili,moja ni usalama na pili ni uchumi,Serengeti uchumi wetu unategemea ufugaji lakini hatujafuga kwa tija’’alisema Waryuba
Awali akisoma Risala kwa mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha mifugo Bi.Rehema koka amesema zoezi la uvishaji Hereni linafanyika ili kutekeleza sheria ya utambuzi,usajiri na ufatiliaji wa mifugo Na.12 ya mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011 ,sera ya taifa ya maendeleo ya mifugo ya mwaka 2006 na ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025,Wilaya ya Serengeti inategemea kuvalisha idadi ya mifugo hereni ikiwa N’gombe 514,660, Punda 5,089,Mbuzi 255,821, Jumla ya Mifugo 964,208.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti