Na.
Goodluck Mwihava
Serengeti
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt.Vincent Mashinji,amezindua rasmi ofisi za uhamiaji wilaya ya Serengeti,Mkoa wa Mara uzinduzii huo ulihudhuriwa na wadau pamoja na wananchi mbalimbali.
Dkt.Mashinji amewashukuru na kuwapongeza wadau waliojitokeza katika kuboresha ofisi hizo za uhamiaji lakini pia aliwakumbusha wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo umuhimu wa ofisi hizo
’’ ofisi za uhamiaji hivi karibuni zimekuwa ni jeshi kamili na hamna nchi inaweza kwenda bila kuwa na idara ya uhamiaji,kwa sababu lazima tuwe na uthibiti wa watu wanaoingia na kutoka nchini na hata wale wanaozaliwa ndani ya nchi hii lazima tuwatambue’’ alisema Dkt.Mashinji.
Pia,aliwakumbusha Wananchi na wageni walikwa kuwa idara ya uhamiaji ina majukumu mengi sana ikiwemo kuwatambua wananchi wote waliopo ndani ya nchi,aliwasisitiza wananchi kutumia ofisi hizo na kufuata taratibu zote za kisheria ili kufanya nchi kuwa salama na kuepuka wahamiaji haramu na changamoto zingine.
‘’Ofisi uhamiaji zinajukumu pia za kuhakikisha kwamba wanaofanya kazi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Watanzania,na wanafanya kazi kwa Maslahi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si vinginevyo’’alisisitiza Mkuu wa wilaya.
Aidha,amewakumbusha raia wakigeni waliopo wilaya Serengeti kupata vibali vya kufanya kazi ndani ya wilaya Serengeti lakini pia wageni wote wanaoingia ndani ya Nchini kutambulika na kufata taratibu zote kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa.
Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Serengeti inaofisi nyingine 3 ambazo ni Serengeti,Seronera,borogonja.Majukumu mengine ya ofisi za uhamiaji ni kutoa elimu ya uhamiaji,kutoa hati za kusafiria,kufanya doria,Upelelezi,Misako,kudhibiti uingiaji wa wageni haramu,kutoa vibali vya walowezi,kuongeza muda kwa wageni pia kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
‘’Ofisi za uhamiaji Serengeti zilianza ukarabati tangu Januari,2022 Kwa muda mrefu tulikuwa tuna jengo chakavu,Tunawashukuru kampuni ya SB Tanzania Limited,Yenye Hotel ya Melia Serengeti waliamua kutusaidia kufanya ukarabati huo’’alisema afisa uhamiaji wilaya ya Serengeti Esia E. Mwakyusa
Akisoma risala kwa mgeni Rasmi afisa uhamiaji Wilaya ameomba kuboreshewa ofisi Zaidi kukidhi matakwa ya kijeshi kwani ofisi hizo bado hazijajitosheleza.Ametoa wito kwa wadau Zaidi kujitokeza kusaidia vitu mbalimbali pamoja na ujenzi wa ofisi za kisasa Zaidi.
Kaimu afisa uhamiaji Mkoa wa Mara Bw.Shabani Kinanda ameshukuru msaada huo wa ukarabati wa jengo hivyo kwani itaongeza morali kwa maafisa na kusaidia katoa huduma kwa wananchi kwa weledi. Nao Wananchi wameshukuru kwa ofisi hizo kwani itasaidia kurahisisha shughuli za uhamiaji.
‘’Tunashukuru kwa ajiri ya uzinduzi wa hili Jengo kwa maana wao ni wadau wakubwa katika kukamilisha zoezi la Nida,katika ugawaji wa vitambulisho vya Taifa kwa sababu bila wao kazi yetu inakwama kwahiyo inamchango mkubwa na tunautambua sana.’’ Alisema Afisa usajiri Wilaya ya Serengeti vitambulisho vya Taifa NIDA Bi.Christina Josinga
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti