Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Serengeti, Mhandisi Juma Hamsini (aliyesimama) ameongoza kikao cha kwanza cha uzinduzi wa Baraza jipya la Madiwani katka kipindi cha 2020 - 2025
Akizungumza katika kikao cha uzinduzi wa Baraza hilo jipya la Madiwani tarehe 11 Desemba 2020, Mhandisi Juma Hamsini amewakumbusha viongozi wote wa halmashauri wakiwemo Wakuu wa Idara kufanya kazi kwa bidii ili kondoa kero mbalimbali kwa wananchi.
Mhandisi Hamsini, amewasisitiza Waheshimiwa madiwani kusimamia miradi na kuwahudumia kwa ukaribu wananchi katika kata zao.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu, ametumia fursa hiyo kuwataka madiwani wote kwenda kuhamasisha na kusimamia Maendeleo ya Serengeti ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na Sekondari kwenye maeneo yao ya uongozi ili kuwezesha wanafunzi wote watakaoripoti Januari 2021 kusoma bila msongamano
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu (aliye nyanyua mkono) akizungumza katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti