Tshs Milioni 60 zajenga Ofisi Mpya ya Serikali ya Kijiji cha Nyichoka
Imewekwa: December 18th, 2017
Serikali ya kijiji cha Nyichoka kutoka Kata ya Kyambahi Wilayani Serengeti yatimiza lengo iliyojiwekea kwa muda mrefu kwa kuwa na ofisi bora. Akiongea na Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mheshimiwa Emmanuel Nyangaka amesema ujenzi huo wa ofisi hiyo umegharimu kiasi cha Tshs 60,852,300 ambapo vyanzo vya fedha hizo ni kutoka mapato inayopata Kijiji kutokana na uhifadhi, ruzuku kutoka Serikalini pamoja na michango ya wananchi. “Kukamilika kwa ofisi hii ni furaha kwetu kwakuwa jengo la zamani lilikuwa ni chakavu sana na vyumba vya ofisi vilikuwa ni vichache” alisema Mheshimiwa Nyangaka.
Bwana Mkome Wambura Mtendaji wa Kata ya Kyambahi amesema kukamilika wa ofisi hiyo sasa kutarahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa ufanisi na utunzaji mzuri wa nyaraka za Serikali.
Jengo la Ofisi mpya za Serikali ya Kijiji cha Nyichoka, Kata ya Kyambahi Wilayani Serengeti
Jengo la Zamani la Ofisi ya Kijiji cha Nyichoka
Serikali ya Kijiji cha Nyichoka sasa inahamia katika ofisi mpya huku ikiwa ni miaka 16 tangu ilipoanza kutumia jengo la zamani.