Mratibu wa Tasaf Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Bi Antusa Swai amewaomba Wanufaika wa Kaya Masikini kupitia Mradi wa Tasaf awamu ya III ambao umeanza 19/04/2021 kuzitumia fedha hizo katika kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya ufugaji pamoja na kilimo ameyasema haya baada ya kukutana na changamoto ya ulevi kwa wanufaika toka Kata ya Morotonga Kitongoji cha Seronga ambacho kimepokea Tsh 2,888,000/=.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Seronga Bwana Buruna Nyawela Lucas amelaani vitendo hivyo kutoka kwa Wananchi wake ambao wanakuja kuchukua fedha hizo wakiwa wamelewa amesema kuwa atawasilisha malalamiko hayo kwenye vikao ili vya Serikali ya Kijiji ili wanufaika ambao wanatumia fedha hizo kwa masuala ya ulevi waondolewe kwenye mpango ili waingizwe wanufaika ambao wana uhitaji zaidi.
Zoezi hio lilimeendelea vizuri katika vitongoji vingine ndani ya Kata za Mamlaka Tarafa ya Rogoro ambapo Kitongoji cha Stand Mpya kimepokea Tsh 2,180,000/= kwa ajili ya wanufaika 42,Kitongoji cha NHC wamepokea Tsh 2,018,000/= kwa ajili ya Kaya 45 huku Kitongoji cha Sedeco wakipokea jumla ya Tsh 2,876,000/= kwa wanufaika 62.
Zoezi hilo la uwasilishaji wa fedha linaendelea mpaka 22/04/2021 katika Kata zingine zilizobaki ambapo walengwa wote ambao wako kwenye mpango watanufaika haya yamesemwa na Mkuu wa Msafara wa Timu ya uwasilishaji wa fedha hizo ambaye pia ni Mkaguzi wa Ndani wa Mahesabu Bwana James Tuniga.
Imeandaliwa
Emmanuel Isyaga Mwita
Afisa Habari -Mahusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
16/04/2021.
instgram:serengeti_sdc_176
facebook:halmashauri ya wilaya ya serengeti
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti