Kampuni ya Utalii ya Nyamoyo Adventure katika kuunga mkono jitihada za serika kukuza sekta ya elimu imeitoa msaada wa mabati katika Shule ya Sekondari Kambarage yatakayo weka mazingira bora ya wanafunzi kujisomea.
akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ndg. Baraka Thobias amesema lengo la kampuni hiyo kutoa msaada wa mabati kwa shule hiyo ni kuonesha jinsi kampuni hiyo inavyothamini elimu kwa watoto hivyo msaada huo utaongeza nguvu katika ujenzi wa madarasa yatakayo chochea usomaji na ujifunzaji wa wanafunzi.
“Leo tumefurahi kukabidhi msaada huu wa mabati kwa Shule ya Sekondari Kambarage ili kuongeza nguvu ya ujenzi wa madarasa ambayo yatatumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita,” alisema Thobias
Aidha, Thobias ameongeza kuwa kutokana na uwepo wa kampuni nyingi za kitalii Wilayani Serengeti ni wakati sasa kwa wananchi kufaidi uwepo wa kampuni hizo kwa kuzishika jamii zinazo zunguka kampuni hizo.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Kambarage wameushukuru uongozi wa kampuni ya Nyamoyo kwa namna ilivyoona umuhimu wa kuisadia shule hiyo kwani kupitia msaada vizazi vijavyo vitafaidika.
Nyamoyo ni mojawapo ya kampuni za kizalendo zinazopatikana ndani ya Wilaya ya Serengeti ambazo zimekuwa chachu ya kukuza sekta ya utalii nchini.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti