Serengeti, Mara
Shule ya Msingi mpya na ya kisasa iliyopo Kata ya Mugumu Wilayani Serengeti Mkoani Mara iliyopewa jina la "SHULE YA MSINGI MUUNGANO" sasa tayari kutumika mwakani baada ya ujenzi kukamilika.
Shule hiyo iliyojengwa kwa Fedha za Mradi wa Boost maarufu kama "FEDHA ZA MAMA" inajumla ya majengo 17 ambapo majengo 14 yakiwa ni madarasa ya shule ya msingi, majengo mawili yakiwa ni shule ya awali huku jengo moja likiwa ni la utawala na matundu 25 ya vyoo.
Ujenzi wa Mradi huo ulianza Mwezi May, 2023 na kukamilika Mwezi September, 2023.
HAKIKA FEDHA ZA MAMA ZIPO SALAMA SERENGETI.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti