Kutokana na Mvua kali iliyoambata na upepo Mkali Kuangusha Miti na kuezua paa za Taasisi na Makazi katika kata ya Natta mnamo tarehe 09 Mei 2022, Kamati ya Ulinzi na usalama(W) ilitembelea Taasisi na wahanga walioathiriwa na Mvua hiyo,Na Mkuu wa Wilaya Serengeti kutoa wito kwa Wadau kujitokeza ili Kutatua changamoto Hiyo kwa pamoja.
Wadau wamejitokeza na kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi kwa kushirikiana na serikali.ambapo Mpaka sasa Miti yote iliyoangukia taasisi imeondolewa na huduma za umeme zimerejea Baada ya TANESCO kuchukua hatua za Haraka.
Aidha,uandaji wa BOQ umekamilika na Zoezi la ujenzi limeanza.Kampuni ya Grumeti Resevers imetoa msaada wa vifaa ujenzi vyenye thamani ya Mil.9 ambavyo ni Mabati 210 na Misumari.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt.Vincet Mashinji amewashukuru Wananchi waliojitokeza kutoa msaada wa Hali na Mali kwa michango na nguvu kazi yao ili kuhakikisha taasisi zinarudi katika hali yake ya kawaida na kuendelea kutoa huduma,Lakini pia amesisitiza kila Mwanafunzi kuwa na Mti na kila kaya kupanda miti katika maeneo yao.
Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Serengeti Ndg.Kivuma H.Msangi amewapongeza wananchi na wadau waliojitokeza kwa kujitoa kuhakikisha hali ya taasisi zinatengemaa.
Mwalimu Mkuu wa Shule Natta Mbisso Ameishukuru Serikali na Wadau waliojitokeza kusaidia kutatua changamoto hiyo ya kuezuliwa kwa kwa madarasa manne.
Nae,Meneja uhusiano wa Kampuni ya Grumeti reserves Bw. David Mwakipesile amesema ‘’Baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wenzetu wa kijiji cha Natta tulikuja na kuona hali ya uharibifu ambao umesababishwa na Janga hili la Mvua na Upepo Mkali,na sisi baada ya kuona tuliona tutoe mchango wetu kama Majirani Hivyo tumetoa Mabati na misumari yake.’’
Ifikapo Siku ya Jumatatu tarehe 16 Mei 2022,Marekebisho katika tasisi yatakuwa yamekamilika na shughuli kuendelea kama kawaida huku tahadhari Zaidi zikiendelea kuchuliwa ili kujikinga na majanga ya aina hayo kwa kupanda miti kwa wingi.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti