Halmashauri ya wilaya ya Serengeti imezindua Rasmi Mkakati wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya elimu Msingi.Ambapo vitabu vitatu vilivyosheheni mikakati hiyo imezindulia na Katibu tawala Wilaya ya Serengeti Ndg.Qamaca C.Qamara, kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti.
Ikiwa ni Takribani Mwezi Mmoja tangu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa kuzindua mkakati huo kitaifa,na hatimaye kuzinduliwa hivi karibuni kimkoa.
Akizinduza mikakati hiyo wa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti ,Katibu tawala Wilaya amewataka wadau hao waelimu kuzingatia yote yaliyokuwepo kwenye mikakati hiyo ili kuweza kuleta ufaulu na mabadiliko yanayotegemewa kitaifa.
Nae, afisa elimu sekondari Mwl.Chatta luleka Amesema kwamba Ofisi ya Rais – TAMISEMI yenye jukumu la kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa sera miongozo ya Elimu ya Msingi na Sekondari imetoa mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa ngazi ya Elimu Msingi ambapo Mkakati huo umegawanyika katika sehemu tatu, sehemu ya kwanza inaonesha mkakati wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya Elimu Msingi, sehemu ya pili ni changamoto katika uboreshaji Elimu Msingi na Sekondari na hatua za kuchukua na sehemu ya tatu inaonesha uteuzi wa viongozi Elimu wa ngazi zote kuanzia katika shule hadi Mkoani.
Ameongeza pia Lengo kuu la sehemu ya kwanza ya mkakati ni kuimarisha uandikishaji, ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya Elimu Msingi.
‘’ Utekelezaji wa mkakati huo unaongozwa na nadharia ya mabadiliko (Theory of change), katika nadharia hiyo hatua ya kwanza ni kuchambua hali halisi ya tatizo ambalo huanza na viashiria vya tatizo, visababishi vya tatizo na athari za tatizo. Hatua ya pili ni kutafuta namna ya kukabili tatizo hilo kwa kuangalia fursa zilizopo katika mazingira ya fursa zilizopo mazingira ya tatizo ambazo zinaweza kutumika kutafuta tatizo husika. Hatua ya tatu ni kupanga mikakati ya kutumia fursa zilizopo kutatua tatizo ikiwa ni pamoja na kupanga utekelezaji wa mkakati, ufuatiliaji na kufanya tathimini endelevu na tathimini tamati‘’Alisema Luleka
Aliongeza kwa kusema Sehemu ya pili ni uboreshaji wa Elimu Msingi na sekondari na hatua za kuchukua sehemu hii inaonesha maboresho ya mifumo ya ufuatiliaji na usimamizi wa utoaji huduma yaliyofanywa, hali ya utoaji wa Elimu msingi na changamoto za uboreshaji wa Elimu na utatuzi wake na Sehemu ya tatu na ya mwisho ni uteuzi wa viongozi wa Elimu wa ngazi zote kuanzia ngazi ya shule, Kata, Halmashauri na Mikoa. Eneo hili limebainisha nafasi, sifa za kimuundo na kiutendaji, muundo wa kamati za mapendekezo ya uteuzi zitakavyofanya uchambuzi na kuwasilisha mapendekezo yake kwenye Mamlaka ya uteuzi. Eneo hili lina sehemu tano, ambapo sehemu ya kwanza ni Mamlaka ya uteuzi wa viongozi, sehemu ya pili ni sifa za viongozi, sehemu ya tatu ni utaratibu wa uteuzi, sehemu ya nne ni uendeshaji wa kamati za mapendekezo ya uteuzi na sehemu ya tano ni majumuisho
Kuwepo kwa mkakati kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza na kundoa changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu Msingi wilayani Serengeti.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti