• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Serengeti yaongoza kitaifa utoaji wa mikopo kwa wanawake na vijana.

Imewekwa: December 28th, 2017

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti yapongezwa kuongoza kitaifa katika utoaji wa mikopo kwa wanawake na vijana kutoka vyanzo vya mapato ya ndani.

Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 28 Disemba 2017 na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Nurdin Babu alipokuwa akizindua Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi pamoja na mafunzo ya ujasiliamali kwa vikundi vya wanawake na vijana katika ukumbi wa Halmashauri.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Mheshimiwa Nurdin Babu

“Nawapongeza viongozi na watendaji wa Halmashauri kwa kutoa mikopo kwa wanawake na vijana na kufanikiwa kuongoza kitaifa, tuendelee kutenga fedha za mikopo kulingana na makusanyo yetu” amesema Mheshimiwa Babu.

Aidha Mheshimiwa Babu amewataka madiwani wote kuchochea maendeleo katika Kata zao kwa kuwahamasisha wananchi kuunda vikundi vya wajasiliamali ili kuweza kupatiwa mikopo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mheshimiwa Juma Porini

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Juma Porini amesema Halmashauri hutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kutoka vyanzo vyake vya ndan vya mapato kwa ajili ya mikopo hiyo huku akitaka vikundi vitumie fedha hizo kuchochea maendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Serengeti. “Kwa mwaka wa fedha 2016/17 Halmashauri yetu imeweza kutoa mikopo yenye thamani ya Tshs 220,000,000 kwa vikundi vya wanawake 43 na vijana 32” alisema Mheshimwa Porini.

 Jumla ya Tshs 103,000,000 zimetolewa kwa vikundi vya wanawake na vijana huku Tsh 63,000,000 ikiwa imetolewa kwa vikundi 20 vya wanawake na Tshs 40,000,000 kwa vikundi 11 vya vijana.

Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Mheshimiwa Marwa Ryoba

Aidha Mbunge wa jimbo la Serengeti ameipongeza Halmashauri kwa kuongoza kitaifa katika utoaji wa mikopo huku akiviahidi vikundi vya wajasiliamali kupatiwa misaada zaidi ya elimu ya ujasiliamali na mikopo.  

Katika mafunzo ya ujasiliamali yaliyokuwa yakitolewa na Idara ya maendeleo ya Jamii Bwana Sunday Wambura Afisa Maendeleo ya Jamii amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia katika shughuli za maendeleo huku akivihimiza vikundi kuanzisha viwanda vidogo dogo ambavyo gharama yake ni ndogo.

“Katika mwakawa fedha 2017/18 Halmashauri yetu imejipanga kutoa awamu mbili za mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana. Leo tunatoa awamu ya kwanza na tutatoa tena awamu nyingine kabla ya kufunga mwaka wa bajeti 2017/18” alisema Bwana Wambura.

Vikundi vya wanawake wajasiliamali wakiwa katika mafunzo


Wanawake na vijana wakiwa katika mafunzo ya ujasiliamali katika ukumbi wa Halmashauri



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI. June 11, 2025
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WADAU WA ZAO LA TUMBAKU WATAKIWA KUZINGATIA MIONGOZO YA KILIMO CHA ZAO LA TUMBAKU ILI KUPATA TIJA YA ZAO HILO.

    June 17, 2025
  • WANANCHI WA KIJIJI CHA PARK NYIGOTI SERENGETI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOKA GRUMETI FUND.

    June 13, 2025
  • GRUMETI FUND YAENDELEA KUGUSA MAISHA YA VIJANA WA KIKE NA KIUME WILAYANI SERENGETI.

    June 04, 2025
  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti