Lishe ya kwanza ya mtoto anapozaliwa ni Maziwa ya Mama.Kwa kutambua hilo dunia imetenga wiki ya unyonyeshaji ambayo ni kila tarehe 1 mpaka 7 agosti ya kila mwaka,ili kuikumbumsha jamii umuhimu,faida na namna bora ya unyonyeshaji.
Unyonyesha wa maziwa ya Mama una faida nyingi na unachangia kwa kiasi kikubwa katika afya ya mtoto kwa kumpatia chakula kinachohitajika kwa ukuaji na maendeleo yake.
Ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya wiki Unyonyeshaji wa maziwa ya mama duniani ,yenye kauli mbiu inayosema ‘’chukua hatua endeleza unyonyeshaji,Elimisha na toa msaada,’’ wilaya ya Serengeti imeendelea kujizatiti kwa kutoa elimu ya unyonyeshaji kwa mama wanao hudhuria katika kliniki lakini pia kipindi cha ujazito,na katika mikutano ya hadhara.
Mtoto huanza kunyonyeshwa katika kipindi kisichozidi saa moja baada ya kuzaliwa ili kuweza kumkinga mtoto tatizo la Manjano Jaundice.Kuepusha vifo vya watoto ,kimkinga mtoto dhini ya magonjwa Lakini pia maziwa ya mama humfanya mtoto kuweza kukua kusaidia katika afya Njema ya akili na mwili.
Unyonyeshaji unafaida mbalimbali kwa Mama,kwani humsaidia mama kutopata hedhi na hivyo kumsaidia kuzuia uwezo wa kupata ujauzito ndani ya miezi 6 ya awali,lakini pia unyonyeshaji wa maziwa pekee usiku na mchana husaidia tumbo la uzazi la mama kurudi katika hali ya kawaida.
Kwa kutambua faida lukuki zilizopo katika kunyonyesha kuanzia kwa mama,mtoto,familia na Taifa kwa ujumla halmashauri ya wilaya ya Serengeti imeendelea kuhakikisha elimu sahihi inawafikai walengwa na Jamii kwa ujumla.Swala la lishe kwa mama pia ni kipaumbele kingine ambacho wilaya imeendelea kusisitiza.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti