Leo tarehe 04.07.2019 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kupitia Idara ya Fedha, imeendesha semina ya mafunzo ya usuluhishi wa kibenki (bank reconciliation) kwa wahasibu wote waliopo katika shule, zahanati pamoja na vituo vya afya vilivyopo wilayani humu, semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmshauri.
Washirika wa semina wakimsikiliza muwezeshaji
Akiongea baada ya mafunzo hayo mwezeshaji ambaye ni Mkuu wa Idara ya Fedha Bw. Itendele Maduhu amesema kuwa semina hii ni ya siku mbili yaani leo na kesho na yana lengo ya kuhakiki taarifa za kibenki pamoja na kuwajengea uwezo wahasibu hao katika utumiaji wa mfumo wa “FARRS”
Bw. Maduhu ameongeza pia kusema kwamba usuluhishi wa kibenki ni hitaji la kisheria kwa kuzingatia sheria ya Memoranda ya fedha ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 2009 hivyo ni lazima kila anayehusika kuhakikisha anasimamia na kutekeleza usuluhishi huo.
Aidha Bw. Maduhu amewasisitiza wahasibu wote kuwa usuluhishi wa kibenki katika mfumo wa “FARRS” uwe unafanyika ndani ya siku kumi (10) kila baada ya Mwezi Kuisha na wazingatie muda, kanuni na taratibu za kifedha zinafatwa ipasavyo.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza muwezeshaji (hayupo pichani) kwa makini
Miongoni wa wahasibu walioshiriki mafunzo hayo Bw. Samson Mgutu (Mhasibu wa shule ya sekondari Nyansurura) amesema kuwa anashukuru uongozi wa halmashauri kwa kufanya semina hiyo kwani wanaamini kuwa itakuwa chachu katika utendaji wao wa kazi hivyo kupitia semina hii watatekeleza kwa wakati yale yote waliyofundishwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zote za kifedha zinafuatwa.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti