Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imefanya mkutano mkuu wa nusu mwaka wa wadau wa maji na usafi wa mazingira leeo tarehe 24.08.2020 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti, ukiwa na lengo la kujadili wapi walipotoka, wapi walipo na wapi wanapokwenda.
Akifungua mkutano huo mkuu wa wilaya ya Serengeti Mhe. Nurdin Babu amesema anawapongeza Wizara ya Maji kupitia RUWASA ngazi ya mkoa na wilaya kwa kuweka utaaratibu wa kuwa na mkutano wa wadau wa maji.
“Ninapenda kuwapongeza Wizara ya Maji kupitia RUWASA ngazi ya Mkoa na Wilaya, kuweka utaratibu huu muhimu wa kuwa na vikao vya wadau wa maji. Kikao hiki cha pili ni muhimu na ndipo mahali ambapo sote tutajitathimini kuanzia tulipotoka, tupo wapi kwa wakati huu na tuanaendelea kwenye hatua ipi” alisema Mh. Babu
Akiendelea kusema Mhe. Babu amaesema kuwa huduma ya maji ni suala la mtambuka kwa kuwa linagusa sekta zote kuanzia kwenye uhitaji, ujenzi, usimamizi na uendelevu wa huduma ya maji. Kwa hiyo kikao hiki cha wadau wa maji, pamoja na mambo mengine lengo lake kuu ni kutuwezesha tujadili kwa kina njia bora itakayowezesha kuimarisha huduma ya maji na kuimarisha usafi wa mazingira katika jamii zetu. Lengo kuwa na miradi endelevu.
Aidha Mhe. Babu amewataka kila mtu kuhakikisha kuwa anazitumia sheria na kuhakikisha kuwa anatambua wajibu na majukumu yake katika kusimamia miradi ya maji. Pia amewaagiza wote wanaosimamia miradi ambayo hadi sasa haijakamilika kuhakikisha inakamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ukiwemo mradi wa maji wa kijiji cha Nyamitita
Naye Meneja wa RUWASA wilaya ya Serengeti Mhandisi Endrew Kisaro amesema kuwa, wakati RUWASA inaanzishwa upatikanaji wa maji katika wilaya hii ulikuwa sawa na asilimia 52 lakini kwa sasa upatikanaji wa maji umepanda hadi kufikia asilimia 59.56 na huku wakitarajia kuwa na upatikanaji wa wa maji kwa asilimia 78.25 hapo baadae
Katika mkutano huo kuliambatana na mada mbali mbali zikiwemo; maboresho ya uendeshaji na usimamizi wa shughuli za sekta ya maji nchi, sheria za maji, fedha za mradi wa maji, uhifadhi wa maji, usafi wa mazingira majumbani na mashuleni, uthibiti wa fedha za miradi na ukaguzi n.k
MATUKIO KATIKA PICHA
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti