Ikiwa ni muendelezo wa utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya Miaka 5,Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) wilayani Serengeti imejadili na kujipanga kuwafikia watoto wote wilayani hapa ambao wanapaswa kupata chanjo ya polio dozi ya 3.
Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya msingi Dkt. Vincent Mashinji ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo hii muhimu ili kuwawezesha kuwa na kinga imara dhidi ya ugonjwa huu wa kupooza.
Aidha,amewataka watoa huduma za Afya kufanya kazi kwa weledi na kujitoa ili kuhakikisha watoto wote waliochini kati miezi 0-59,wanapata chanjo hiyo ili kujikinga na ugonjwa hatari.
Kikao hiki Muhimu cha kujadili kampeni dhidi ya ugonjwa wa polio kimehudhuriwa na Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Serengeti Ndg Kivuma Msangi,Mganga mkuu Wilaya ya Serengeti Dkt.Emillian Donald ,Kamati ya ulinzi na usalama,baadhi ya watumishi wa afya.Kauli mbiu ya Kampeni hii endelevu Kila tone la chanjo ya polio itaweka Tanzania salama,Mpe Chanjo Okoa Maisha.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti