Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti tumepokea Kompyuta (Desktop) tano na Printa tano kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, kwa ajili ya Vituo vya afya vitano ambavyo ni Natta, Iramba, Kebanchebanche, Kemgesi na Machochwe.Tunategemea vifaa hivi vitaongeza thamani katika juhudi za serikali za kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya katika vituo tajwa.
Kabla ya Kukabidhi sehemu ya msaada wa vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mh. Juma Porini Keya (Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya) aliishukuru sana Serikali kwa mchango wa vifaa hivyo.
Mh. Porini aliongeza kwa kusema “Naamini watazitumia vizuri kuhakikisha kwamba lengo na makusudio ya kuzipata hizi mashine wanatekeleza kwa hiyo naomba wazitunze vizuri sana lakini pia zisiwepo kama mapambo kuhakikisha wanazitumia na kadri ya maelekezo yalivyotolewa” alisema
Kwa upande wao Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Natta DKT Crisantus Magori na Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Iramba DKT Golobana Wellah Wakipokea mashine hizo kwa niaba ya Vituo vyote Vitano walisema wanaishukuru sana Serikali kupitia OR TAMISEMI kwa msaada huu japo bado kuna uhaba wa vifaa kama hivyo lakini wanashukuru hata kwa hivi walivyovipata sasa.
DKT Crisantus Magori mwenye shati Jeupe pamoja na DKT Emiliana Donald (kaimu Mganga mkuu wa Wilaya) mwenye Blauzi ya pinki wakipokea sehemu ya vifaa vilivyotolewa na Serikali kupitia OR TAMISEMI kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Juma Porini Mwenye shati la Kijivu
DKT Golobana Wellah (kushoto) pamoja na DKT Emiliana Donald (kaimu Mganga mkuu wa Wilaya) mwenye Blauzi ya pinki wakipokea sehemu ya vifaa vilivyotolewa na Serikali kupitia OR TAMISEMI kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Juma Porini Mwenye shati la Kijivu
Picha ya pamoja baada ya halfa fupi ya kupokea vifaa
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti