Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Ayub Makuruma amelitaka shirika la "Hope for girls and women" kuongeza elimu kwa wakazi wa Wilaya ya serengeti juu ya madhara ya ukeketaji na ukatili kwa wanawake.
akizungumza wakatika wa mkutano wa baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya serengeti Mhe. Makuruma amesema ili vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake viweze kufikia kikomo ni vyema kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wajue madhara yake.
"Endapo mtaongeza elimu hata mkitumia nguvu kidogo watu wataelewa haraka kuliko kutumia nguvu nyingi alafu bado matokeo yanakuwa mabaya" alisema Mhe. Makuruma.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls shirika linalojihusisha na kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake amesema shirika hilo kinaendelea kuweka juhudi ya kutoa elimu pamoja na kuwasaidia watoto wa kike wanao kumbana na kadhia ya ukeketaji.
Katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo kamati za kudumu zimepata fursa ya kuwasikisha taarifa za utekelezaji wa shughuli zilizofanywa na Halmashauri kwa kipindi chote cha robo ya Kwanza (Julai - Septemba 2023).
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti