Ikiwa ni Miaka 24 tangu Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Bado anaendelea kukumbukwa kwa juhudi na harakati zake za kuleta Amani na kufanikisha Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika na Bara la Afrika kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti inaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote katika kumbukizi hii ya kifo cha baba wa taifa.
Baba wa taifa anakumbukukwa kwa juhudi zake za kupigania Uhuru na kuwaunganisha Watanzania pamoja na Falsafa yake ya kutokomeza Maadui watatu wa Taifa hili yaani Ujinga, Umasikini na Maradhi.
Vilevile katika kumbukizi ya siku hii, tukumbushane wosia wake kuhusu maendeleo: "Ili tuendelee, tunahitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi, na Uongozi Bora".
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti