Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula (MB) ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya pango ya ardhi, amebainisha hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya hii leo tarehe 20/02/2019 katika ukumbi wa halmashauri.
Ziara yake iliyolenga kufanya uhamasishaji na ufuatiliaji wa makusanyo ya kodi ya pango ya ardhi kwa nchi nzima.
Mh. Naibu Waziri alibainisha kuwa katika Halmashauri ya Serengeti tupo nyuma sana katika ukusanyaji wa kodi ya pango. “Serengeti mpo nyuma sana Lengo lenu mlijiwekea Milioni mia saba ishirini lakini mpaka tunafikia Februari leo tulipo hapa na hii robo ya tatu mna asilimia kumi na saba mmebakiza robo moja sasa ni lini mtafikisha asilimia 90? Kwa sababu hadi kufikia Disemba mlitakiwa kuwa na asilimia hamsini katika ukusanyaji wa lengo mliojiwekea” Alisema Mh. Mabula
“Lakini katika hesabu zenu Milioni 126.6 kati ya milioni 720 bado kazi haijafanyika bado mna jukumu kubwa la kuweza kufikia lengo” aliongezea Mh. Mabula
Wakati huo huo ameagiza wale wadaiwa sugu wote waliopelekewa ilani ya kulipa kodi na muda wa ilani umekwisha wafikishwe katika Baraza la Ardhi ili hatua za kisheria zifuate. Aidhan ameagiza oia taasisi zote zilizopo wilayani zipimiwe maeneo yao na waanze kulipa kodi mara moja.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti