Sifa hizo zimemwagiwa na Mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2019 Ndg. Mzee Mkongea Ali wakati alipokuwa akitembelea miradi ya maendeleo iliyotengwa kwa ajili ya mbio za mwenge wa uhuru wilaya Serengeti ili kuzindua, kuweka jiwe la msingi na kutembelea.
Mwenge wa uhuru katika wilaya ya Serengeti umeweza kupokelewa leo tarehe 05/06/2019 katika kijiji cha Nyansurura, Kata ya Nyansurura, Tarafa ya Ikorongo kutoka wilaya ya Tarime na Kauli mbiu ya Mwaka huu ikiwa “MAJI NI HAKI YA KILA MTU, TUTUNZE VYANZO VYAKE NA TUKUMBUKE KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA”
Mwenge wa Uhuru umeweza kutembelea miradi ya maendeleo tisa yenye jumla ya thamani ya Tsh. 1,838,990,684.80 ikiwa michango ya serikali kuu Tshs 893,740,251.80, michango ya halmashauri Tshs 73,797,760.00 michango ya wananchi Tshs 643,514,673.00 na michango ya wahisani Tshs 227,938,000.00.
Mwenge wa uhuru uliweza kutembelea na kuzindua miradi mitano ambayo ni mradi wa nyumba ya walimu “Six in one” na Klabu ya Mapambano dhidi ya Rushwa katika Shule ya Sekondari Mama Maria Nyerere, vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Msingi Getarungu, mradi wa kisima cha maji katika Kijiji cha Makundusi kata ya Natta, mradi wa Shule ya Sekondari Makundusi Kata ya Natta na Mradi wa kitalu cha Miti makao makuu ya wilaya.
Pia mwenge wa uhuru uliweza kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi mitatu ambayo ni mradi wa Kiwanda cha Alizeti katika Kijiji cha Kenyana, mradi wa jengo la wodi ya wazazi Zahanati ya Kenyana Kijiji cha Kenyana na mradi wa uzio wa Mnada wa mifugo Mugumu Mjini
Vilevile Mwenge wa uhuru umeweza kutembelea barabara ya lami ya Kilomita 1.3 iliyopo Mugumu Mjini.
Aidha Ndg. Mzee amesisitiza kuwa miradi yote iliyotolewa ushauri ihakikishwe inarekebishwa kwa wakati uliopendekezwa
Naye Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Ndg. Nurdin Babu ameahidi kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na wataalamu wote kuhakikisha kuwa ushauri wote uliotolewa kwenye miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukabidhiwa kesho tarehe 06/06/2019 Mkoani Arusha katika Kijiji cha Ololosokwan na Mkuu wa Mkoa wa Mara Ndg. Adamu Kighoma Malima
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti