Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mheshimiwa Jacob Bega na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Ayub Mwita Makuruma wameendelea na ziara katika Kata za Kebanchabancha na Nyamoko ambako wameendelea na zoezi la kuhamasisha shughuli za Maendeleo katika Kata hizo kulingana na ratiba yao walivyopanga.
Wakiwa Kata ya Kebanchabancha walipokelewa na Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Chacha Matiko pamoja na Wajumbe wa WDC wa kata hiyo ambapo pia taarifa za miradi inayotekelezwa ndani ya Kata ilisomwa pamoja na kuelezea mafanikio yaliyo ndani ya Kata hiyo lakini changamoto ambazo wanakutana nazo katika kutekeleza miradi yao ndani ya Kata yao.
Mheshimiwa Chacha Matiko amewaeleza viongozi hao miradi inayotekelezwa ndani ya Kata hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Shule mpya ya Kebanchabancha ambayo inajengwa na makundi( rika esaigha) ambayo mpaka sasa tayari wameshafikia hatua ya kupaua alitumia nafasi hio pia kumshukuru Mwenyekiti wa Halmashauri Ayub Mwita Makuruma pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhandisi Juma Hamsini kwa kuwapelekea vifaa vya madukani kama Mabati,Mbao,Saruji ambazo kwa kiasi kikubwa zimewasaidia kukamilisha lakini pia amewashukuru Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Ndugu Joel Mwita na Afisa Elimu Kata hiyo Ndugu Adam Nyakimori kwa kazi nzuri ya kusimamia mradi huo wa ujenzi wa Shule hiyo mpya ya Sekondari.
Ziara hiyo iliendelea ambapo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Watalaam toka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ilifika Kata ya Nyamoko na kupokelewa na Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Bugi Mwita Mrimi ambapo pia aliwashukuru kwa kufika.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi alipokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ndani ya Kata hiyo ambapo kwa sasa tayari wametnga hekari 8 kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Masangura kwani wananchi wa Kijiji hicho bado wako nyumba kimaendeleo.
Mheshimiwa Bugi alitumia nafasi hiyo kuelezea changamoto walizonazo wananchi wa Kata ya Nyamoko ambapo alitoa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa hasa kwa Shule ya Kwitete pia Shule ya Nyangwe wana shida hiyo japo kwa sasa tayari wameanza ujenzi wa madarasa na changamoto nyingine iko Masangura ambapo miundo mbinu ya barabara sio mizuri kunafikika lakini kwa shida.
Mwisho aliwashukuru viongozi wa Halmashauri kwa kuhakikisha wanapata Mbati 120,Saruji Mifuko 50 pamoja na Milioni 12 ambazo zimetolewa na Halmashauri kwa ajili ya Ngarawani Sekondari.
Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano-Tehama
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
01/03/2021
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti