Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Ayub Mwita Makuruma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawe na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Serengeti Mhandisi Juma Hamsini 18/02/2021 wamefanya Mkutano na Waandishi wa Habari lengo ikiwa ni kukanusha taarifa ya upotevu wa Mapato ya Halmashauri.
Wakizungumza na Waandishi hao katika Mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi ya Mkurugenzi ambao pia umehusisha Wakuu Idara mbali mbali toka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kwa pamoja wamesema taarifa hizo za upotevu wa Mapato kwa 80% ni za uwongo na zenye lengo la kuichafua Halmashauri ya Wilaya Serengeti kwani Taarifa hio ilikunuliwa kwenye Kikao cha Bajeti ikiwa ni Kikao cha Kawaida cha Bajeti ambapo Madiwani walizingumzia hali ya Ukusanyaji Mapato pamoja na kuibua vyanzo vingine vya Mapato na pia kuangalia ukusanyaji wa Ushuru katika vizuizi vya Nyansurura pamoja kile cha Issenye.
Taarifa ilioandikwa na Mtandao Jamii Forum ilikuwa ni Taarifa ya kupotosha kwani kama ni kweli 80% yanapotea basi Halmashauri hio ya Serengeti ingekuwa imepata Hati chafu jambo ambalo halijawahi kutokea na hata hivo walisisitiza kuwa wako Makini katika masuala mazima ya Ukusanyaji ya Ndani kama mwongozo umavosema wa ukusanyaji Mapato pamoja na Ushuru wa Minada pamoja na makusanyo mengine.
Mkurugenzi Mtendaji amethibitisha kuwa hakukuwa na hoja hio kwenye Kikao na wala Madiwani hakuzungumza hoja ya namna hio hivo Wananachi wawe watulivu kwani bado Halmashauri inakusanya Ushuru vizuri ambao ndio chachu ya ufanyaji shughuli za Maendeleo ndani ya Halmashauri katika Mkutuno huo Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Juma Hamsini alibainisha Miradi baadhi ambayo imetokanana ukusanyaji wa Mapato ya ndani ni pamoja na Ujenzi wa Hospital ya Wilaya Serengeti, Ujenzi wa Stend Mpya ya Mabasi Mugumu lakini kuongezeka kwa Shule za Msingi toka 103 hadi 140 huku shule za Sekondari za Umma zikivuka toka 16 mpaka kufikia 40.
Hata hivyo Mheshimiwa Makuruma na Mhandisi Hamsini wamemaliza kwa kusema kuwa Halmashauri iko vizuri katika ukusanyajina hakuna hata senti moja inayopotea kwani zote zinakusanywa kwa mfumo wa kisasa hivyo wananchi waendelee kuwa na Imani na Halmashauri yao na wazidi kuchapa kazi bila wasiwasi.
Imetolewa
Afisa Habari- Mahusiano
Emmanuel Isyaga Mwita
Halmashauri ya Wilaya Serengeti.
ReplyForward |
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti